Rasta ateuliwa Mwanasheria Mkuu wa Malawi aapishwa, baadhi ya maneno kwenye kiapo agoma kuyatamka. Jaji amsainisha kiapo. Je, ni sahihi kisheria?

Rasta ateuliwa Mwanasheria Mkuu wa Malawi aapishwa, baadhi ya maneno kwenye kiapo agoma kuyatamka. Jaji amsainisha kiapo. Je, ni sahihi kisheria?

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Rastafarian ateuliwa na Raisi mpya Mchungaji Chikwera kuwa mwanashria mkuu wa serikali ya Malawi aapishwa kwa Biblia watu wamshangaa huyo Rasta akiapa kwa Biblia.

Maneno mengine kwenye kiapo anayeapa agoma kuyatamka Jaji muapishaji ajikausha na kupotezea ni kituko fulani hivi

Wanasheria alichofanya huyo Jaji muapishaji ni sahihi kumsainisha kiapo mwenye kuapa kiapo ambacho hajatamka maneno yote ya kiapo kikamilifu?

Naomba wabobezi wa Sheria shusheni nondo .Mtu aki skip maneno kwenye kiapo kuyatamka au kuyabadilisha nje ya yale anayotamka Jaji ayaseme kiapo kinakuwa valid?

INATEGEMEA AMEAMKAJE mh. Jaji siku hio.
Sielewi mfano hapo Jaji anasema sema "SWEAR THAT " Muapaji anachenga anasema " AFFIRM THAT" hatamki Jaji alichosema anatunga maneno yake na Jaji kakausha!!!! hicho kinakuwa sio kiapo kile cha jaji,Muapaji katunga kiapo chake hapo je ni sahihi?
 
Endeleeni kudharau wavuta bangi maana hata wanao wawaidia huko hamjui kama wanavuta au laa.
Hili swali ni kwa learned brothers and sisters wanasheria sio wavuta bangi wa ufipa liko juu ya uwezo wako hili waache wataalamu waje wajibu
 
The point ni kwamba ame sign kiapo. Hata Obama alimung'unya/hakuyatamka maneno fulani wakati wa kuapishwa lakini ali sign kiapo chenye maneno yale ambayo hakuyatamka.

Na kama kiapo hakikuzingatia imani yake na katiba hailazimishi kiwa na imani hiyo hapana shida, unakwepa maneno.
 
Kama kwenye kiapo katamka "naapa kuitunza na kuiheshimu katiba ya malawi" mi nadhani hamna shida kabisa. Maana nao nadhani serikali yao haina dini
 
Sielewi mfano hapo Jaji anasema sema "SWEAR THAT " Muapaji anachenga anasema " AFFIRM THAT" hatamki Jaji alichosema anatunga maneno yake na Jaji kakausha!!!! hicho kinakuwa sio kiapo kile cha jaji,Muapaji katunga kiapo chake hapo je ni sahihi?

Bora huyo kaweka ya kwake, nyie jamaa mnatamka yale yale lakini mnakuja kuikanyaga biblia na katiba.
 
Sielewi mfano hapo Jaji anasema sema "SWEAR THAT " Muapaji anachenga anasema " AFFIRM THAT" hatamki Jaji alichosema anatunga maneno yake na Jaji kakausha!!!! hicho kinakuwa sio kiapo kile cha jaji,Muapaji katunga kiapo chake hapo je ni sahihi?
Kwani amesaini kiapo gani?
 
Kama kwenye kiapo katamka "naapa kuitunza na kuiheshimu katiba ya malawi" mi nadhani hamna shida kabisa. Maana nao nadhani serikali yao haina dini
hakusema naapa alisema I AFFIRM hakusema I SWEAR!! Rudia kusikiliza la kuapa hajatamka!!
 
Kwani amesaini kiapo gani?
Sasa issue kama ni kusaini tu kuna sababu gani aapishwe na kutamka kwenye public si angepelekewa chumbani akasaini kwa mkewe
 
Back
Top Bottom