Ratiba hii TFF mnaziongozea mzigo timu

libeva

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2015
Posts
4,465
Reaction score
3,615
TFF mnapaswa kuzionea huruma timu zinazo shiriki ligi kuu, haingii akilini Yanga wapo kanda ya ziwa wiki mbili kwa mechi mbili Yanga kacheza na Mwadui tar.17/09 mechi ijayo tar.24/09 kwa nn hamkupanga wacheze tar 21/09 ili kuokoa ghalama za timu kukaa hotelini? Yaani wiki mbili mechi mbili kwa nini timu inavyo enda ukanda huo isimalize mechi zao zote huko?
 
Wakipanga mechi za katikati ya wiki mnalalamika, wakipanga weekend mpaka weekend vilevile mnalalamika.
 

Na nyie muwe mnajiongeza basi " sometimes ". Kwanza yakupasa ujue kuwa Simba na Yanga ni brands kubwa hapa Tanzania na ambazo zina fan base ya kutosha hivyo hata Waandaaji nao huwapangia kucheza Weekends mechi nyingi hasa za Mikoani ili kuwapata Mashabiki wengi ambao kimsingi ukiwawekea mechi za hawa Country Titans Weekend watakaoingia ni Watu wachache mno hasa kutokana na mfumo wa maisha wa Watu wa Mikoani ambao haufanani na huu wa Dar au Arusha au Mwanza. Na ukumbuke pia kuwa TFF nao macho yao yako hapo hapo katika hizi Timu mbili ili wajipatie " mtonyo " wa Kiingilio na waweze kuendeshea shughuli zao na maisha yaende.

Mwisho kabisa yakupasa ujue tofauti hii kisha utafakari Wenzetu Ulaya huko FA ( Football Associations ) zao ndizo zinasimamia Vilabu ila kwa hapa Tanzania Vilabu vikubwa viwili Simba na Yanga ndiyo vinaisimamia, kuiongoza na kuiburuza itakavyo TFF ( Tanzania Football Federation )
 
Wakipanga mechi za katikati ya wiki mnalalamika, wakipanga weekend mpaka weekend vilevile mnalalamika.
Angalia umbali mfano Ndanda itoke Mtwara ikae kanda ya ziwa wiki 2 kwa mechi 2 hii sio fair
 
Mara ngapi tumeona inapangwa ratiba ya katikati ya wiki halafu kila mdau anapiga kelele
 
Huko ulaya ilitokea pia timu moja maarufu chini ya Ferguson ilikuwa inaiendesha TFF ya huko na marefa wao, baada ya kuondoka sasa timu inashindana kwa haki na wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…