Ratiba na chanjo za kuzingatia katika ufugaji

Ratiba na chanjo za kuzingatia katika ufugaji

theriogenology

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2016
Posts
8,748
Reaction score
15,681
RATIBA NA CHANJO ZA KUZINGATIA KATIKA UFUGAJI
Vitu vya kuzingatia kabla ya kuchanja mifugo yako;
> Epuka kuchanja mnyama mgonjwa maana kufanya hivyo utachangia kumpoteza mapema
> Mnyama ambaye kinga imeshuka na yupo kwenye dozi ya matibabu asipewe chanjo
> Epuka kumpa mnyama stress baada ya kuchanjwa hakikisha anakaa katika eneo la utulivu
> Usimchanje mnyama ambaye mwenye uchafu kwenye ngozi au kuwa na unyevuunyevu katika ngozi
> Usichangie sindano kutoka kwa mnyama mmoja kwenda kwa mnyama mwingine hakikisha kila mnyama anatumia sindano yake
> Baada ya kuchanganya dawa hakikisha unatikisa vizuri ili iwe katika mchanganyo mzuri kabla ya kuchanja mifugo yako
> Chanjo ihifadhiwe katika mazingira mazuri kama ilivyoshauriwa na mwongozo kutoka kiwandani
> Ikitokea umejichoma kwa bahati mbaya na sindano ambayo ipo na dawa hakikisha unamwona daktari mapema maana chanjo nyingine ni hatari ambayo huweza kukupelekea kupoteza mkono wako
> Unapokuwa unachanja mifugo katika makundi kumbuka kuanzia kwa wadogo na kwenda kwa wakubwa
> Vifungasho ambayo hubeba chanjo( live vaccine) huwa vina hatari hivyo baada ya kuchoma chanjo unashauriwa kuvitekeza katika njia iliyo salama

Baada ya kuona vitu vya kuzingatia kabla na baada ya kuchanja mifugo yako ningependa kugusia kidogo chanjo muhimu ambazo wewe mfugaji unashauriwa kuwapa mifugo wako ili kuwa kinga na magonjwa yanayosababishwa na virusi na bakteria hatari ambao huweza kukusababishia hasara wewe kama mfugaji na kwa kuanza ningependa kuanza na Ruminants hapa nazungumzia ng'ombe mbuzi na kondoo ikifuatiwa na jamii ya ndege na kumalizia na Mbwa;

1. Ruminants ( Ng'ombe, mbuzi na kondoo)
a) Anthrax vaccine ( kimeta)
> Ng'ombe huchanjwa akifikisha umri wa miezi mitatu na kuendelea na baada ya kuchanja inashauriwa kurudia kila baada ya mwaka mmoja
> Baada ya kuchanja kinga hutengemaa baada ya siku ya 10 na unashauriwa baada ya kuchoma usiwachome ng'ombe wako dawa ya antibiotic kwa wiki 4
> unashauriwa usitumie maziwa au nyama ya ng'ombe aliechanjwa mpaka pale wiki6 zitakapoisha

b) Brucellosis vaccine
> Mara nyingi ugonjwa huu husababishwa ugumba au mimba kutoka kwa ng'ombe na hivyo kukuletea hasara wewe mfugaji
> Kuna aina mbili za chanjo nazo ni strain 19 (S19) na strain 45/20 (S45/20) na unasgauriwa usichanje ng'ombe dume kwa kutumia s19
> Ng'ombe huchanjwa wakiwa na umri kuanzia miezi miwili na chanjo inadumu kwa muda wa miaka 7
c) Contagious bovine pleuropneuma vaccine
> Ng'ombe Huchanjwa pale wanapofikisha umri wa zaidi ya miezi 6 na kinga huanza kutengemaa wiki 3 baada ya kuwapa chanjo
> Unashauriwa kurudia kila baada ya mwaka mmoja

d) Contagious caprine pleuro pneumonia vaccine
> Mbuzi huchanjwa baada ya kufikisha umri wa miezi 6 na hurudiwa kila baada ya mwaka

e) Neonatal calf diarrhoea vaccine
> Ng'ombe na mtamba mwenye mimba hutakiwa kuchanjwa wiki 12 hadi 14 kabla ya kuzaa na hii itawakinga ndama kutoka kwa ugonjwa huo

f) Lumpy skin disease ( LSD)
> Unashauriwa kuwachanja ng'ombe wanapofikisha umri zaidi ya miezi 6 na kinga hutengemaa ya 8 baada ya kuwachanja
> Chanjo hii hudumu kwa muda wa miaka 2
g) Foot and mouth disease vaccine
> Ng'ombe hutakiwa kupewa chanjo mara mbili kwa miezi 6 ya mwanzo na kinga hujengeka wiki 2 hadi 3 baada ya kuchanja
> Unashauriwa kuchanja kila baada ya mwaka mmoja

h) Pes des pestis vaccine
> Mbuzi hupewa chanjo hii wanapofikisha umri wa miezi 6 na kinga huimarika siku ya nane baada ya kuwachanja na inakaa maisha yake yote

2. Kuku
a) coccidiosis vaccine
> Hupewa kwenye maji kuanzia siku ya 5-7 na kwa broiler dozi mmoja inawatosha na kwa kuku wa mayai unashauriwa kurudia

b) Fowl pox vaccine ( ndui)
> Kwa sehemu ambayo ugonjwa sio tatizo kubwa unashauriwa kuwachanja wiki ya nane na kurudia kila baada ya mwaka mmoja
> Kwa sehemu ambayo ugonjwa huu ni sugu unashauriwa kuwachanja wiki 3 na kuridia baada ya miezi 3 na baadae unawapa kila baada ya mwaka

c) Fowl typhoid vaccine
> Kuku wapewe chanjo wanapofikisha umri wa wiki 6 na rudia baada ya wiki ya 12
> Kinga hujengeka baada ya siku 10 na unashauriwa kurudia kuwapa chanjo kila baada ya miezi 6-8

e) Mareks vaccine
> Hupewa katika hatchery siku ya kwanza na huweza rudiwa kuku wakifikisha wiki 3 na unashauriwa kuwachoma nyuma ya shingo chini ya ngozi

f) Newcastle vaccine
> Pitia makala yangu ambayo nimeilezea kwa undani zaidi.

3. Mbwa
a) Mbwa huchanjwa kuwakinga na magonjwa ya virus na bakteria na tunawachanja kuwakinga na magonjwa yafuatayo ; Distemper, Hepatitis, Leptospirosis, parvo virus infection, Parainfluenza virus na rabies

★ Ratiba ya uchanjaji mbwa;
Wiki 6 - DHPPi
Wiki 9 - DHPPi + L
Wiki 12 - DHPPi
Wiki 16 - DHPPi + R

> Baada ya hapo chanjo hurudiwa kila baada ya miezi 12
> Na kwa mbwa wadogo ( Puppy) hupewa dawa ya minyoo wakiwa na wiki 2..4...6...8... na wiki ya kumi na mbili huchomwa dawa kuzuia minyoo inayoshambulia moyo na baada ya hapo hutakiwa kupewa dawa ya minyoo kila baada ya miezi 3.


★ Ratiba ya chanjo
kwa kuku
> Siku ya saba chanjo ya Kideri ( Newcastle) dozi ya kwanza kwa njia ya tone kwa jicho
> Siku ya kumi chanjo ya gumboro dozi ya kwanza kwenye maji
> Siku ya ishirini na moja chanjo ya kideri dozi ya pili kwa njia ya tone kwenye jicho
> Wiki ya nne chanjo ya gumboro dozi ya pili kwenye maji
> Wiki ya sita chanjo ya gumboro dozi ya 3 kwenye maji
> Wiki ya 8 Chanjo ya kideri dozi ya tatu kwa njia ya tone
> Wiki ya kumi chanjo ya fowl typhoid kwenye maji
> Wiki ya kumi na mbili chanjo ya ndui ( fowlpox) njia ni kwenye bawa
> Mwezi wa tano chanjo ya kideri dozi ya nne kwa njia ya tone kwenye jicho
Zingatia:
> Rudia chanjo ya kideri kila baada ya miezi miwili na wape dawa za minyoo kuku wako baada ya kufikisha umri wa wiki 8 na rudia kila mwezi.
> Hakikisha maji unayochanganyia chanjo hayana chlorine hivyo unaweza tumia maji ya mvua au kuchemsha maji ya bomba na hivyo kuchanganya dawa.
> Epuka kufuga kwa mazoea na kuwatafuta wataalamu wa mifugo ( Veterinarian) ili waweze kukupa ushauri ulio bora kukuwezesha wewe mfugaji kunufaika na ufugaji.
> Tutafute nasi tutakuchanjia mifugo yako kwa bei nafuu na utakuwa chini ya uangalizi wetu kwa miaka yote ya ufuagaji wako.
Imeandaliwa na C.EO:
JM VeterinaryCentre(JMVC)
Phone: +255686236365
 
Da nimefurahi kwa ufafanuzi wako nitakutafuta mi Niko singida
 
Back
Top Bottom