Raundi ya 23 Epl leo..chelsea vs Leicester

Raundi ya 23 Epl leo..chelsea vs Leicester

Dkileo

Member
Joined
May 23, 2017
Posts
51
Reaction score
46
Baada ya suluhu dhidi ya Arsenal leo Chelsea wanarudi darajani kupambana na Leicester ambayo tokea Claud Puel ameichukua imekuwa na matokeo ya kuridhisha..Chelsea hawapo katika situation nzuri haswa kwa mshambuliaji wao Alvaro Morata ambaye ameshambuliwa vikali na mashabiki kwa kukosa nafasi za wazi…Alikosa nafasi za wazi Zaidi ya mbili katika mechi ya mzunguko wa 22 dhidi ya Arsenal…Ambapo Chelsea walitoshana nguvu ya bila kufungana na Arsenal

Bado Conte hajapata jibu katika sehemu ya kiungo..Hajafahamu ni nani kati ya Bakayoko na Drinkwater aanze na kante na fabregas…mara nyingi amekuwa akimuanzisha Bakayoko ambaye anaonekana kuwa mzito….

Usajili mpya Rose Barkley anaweza kufiti kwenye hiyo nafasi vizuri lakini kwa mujibu wa Conte, Barkley hato weza kucheza mechi ya leo



Antonio conte amekuwa katika majibizano mazito dhidi ya Jose Mourinho siku za karibuni..Ni kawaida Mourinho kuwa na mabishano haswa katika kipindi hiki ambacho ni kigumu na muhimu sana kwa wapinzani wake..Jose amekuwa akitumia kejeli ili kuwaharibu kisaikolojia wapinzani wake..Nakumbuka Jose ameshasumbuana sana na Wenger…

Baada ya Puel kuichukua timu amebadili mfumo kidogo..Amekuwa hatumii namba tisa wawili kama ilivyokuwa kwa shakespeare na Ranieri..Yeye amekuwa akimuweka Vardy mbele huku nyuma yake kukiwa na Damarai Gray,Albrighton na Mahrez…

Adrien Silva usajili ambao ulishindwa kukamilika kipindi cha majira ya joto ambapo walichelewa kwa sekunde 14 leo anaweza kucheza..

Spurs watawakaribisha Everton..Mechi nyingine kali sana siku ya leo..

Nicheki insta @dickykileo
 
Back
Top Bottom