Wakili Madeleka: Huwezi KUMVUNJIA MTU NYUMBA YAKE bila KUMLIPA FIDIA, ili ujenge BARABARA, halafu ukamwambia hayo ni “MAENDELEO YAKE”, asubiri “UTAMLIPA BAADAE”. Sasa unataka AKAISHI WAPI NA FAMILIA YAKE? Huu ni UKATILI ambao HAUKUBALIKI. Serikali ILIPE FIDIA za watu, tena STAHIKI.
Pia soma > Rais Samia: Mnaotudai fidia kuweni na subira tumalize miradi ya maendeleo kwanza ndipo tuwalipe
========
Rais Samia: Tunajua maeneo ambayo miradi inajegwa ni ameneo ya watu lakini tunachokifanya ni maendeleo ya watu, ni maendeleo yenu. Hatukatai kulipa fidia lakini tunapojenga mradi, fedha hizi ni za kudunduliza, kwahiyo tunajenga mradi kwanza wananchi wanufaike halafu tunakuja kuangalia mambo ya fidia.
Kwahiyo kwa wale wote wanaotudaia fidia zao kwa maendeleo yao wenyewe tunaomba muwe na subira, tuacheni tumalize mambo ya maendeleo wananchi wengi wafaidike, halafu tutaangalia mambo ya fidia.
Sasa kuna maeneo watu wanazuia kabisa mradi usipite kwasababu hajapewa fidia, niwaombe sana wananchi, miradi hii si kwa faida ya Serikali kuu, ni kwa faida ya Taifa letu, kwahiyo tuacheni tufanye miradi, mambo ya fidia mimi nawahakikishia hatanyimwa mtu haki yake.
Tukiwa tayari tuwalipa fidia, kwahiyo niwaombe sana wananchi acheni miradi ijengwe kwa manufaa yenu na fidia zitakuja zitalipwa.