Rav 4 kilitime inagonga, miguu ya mbele nimebadilisha shockup na stablizer link lakini bado inagonga

Ukifanya yooote hayo ikashindikana. Nenda kaangalie bearing. Huwa nazo kwa RAV4 Zikishapata shida sana zinakuwa zinacheza na kusababisha kugonga.
 
Aaaargh we, Madaktari wanatukanwa sana tena mpaka kuhoji vyuo walivyosoma.
 
Tairi ya gari inaunganishwa na body na vitu vingi
1.control arms/wishbone-hizi zina bushes,bush zikiisha utasikia matairi yanagonga ukiingia barabara mbovu
2.ball joints-zikichoka gari itagonga ukichelewa zinachomoka..
Pia zikidondoka lock za disk pad,hivyo hupelekea disk pad kugonga gonga kwenye roter disk na kupelekea kupiga kelele sana.
 
Rav 4 kilitime inagonga, miguu ya mbele nimebadilisha shockup na stablizer link lakini bado inagonga, naombeni msaada wadau tatizo ni nini?
Lete mrejesho Jombaaa.
Ulifanyeje tatizo likaisha. Ushauri ukipewa, jitahidi kutoa shukrani
 
Tairi ya gari inaunganishwa na body na vitu vingi
1.control arms/wishbone-hizi zina bushes,bush zikiisha utasikia matairi yanagonga ukiingia barabara mbovu
2.ball joints-zikichoka gari itagonga ukichelewa zinachomoka...
upo sawa kabisa enginer coz ndo kitu tunacho kifanya na tuna uelewaa nacho. SALUTE
 
Tatizo la mafundi wetu hawako competent kwa kitu kimoja...

Fundi mmoja huyo huyo anataka awe fundi wa injini, geabox, umeme, rangi, decorations,brake system, AC, Music, Cooling system, Suspension system na kadhalika....hapo lazima fundi awe shallow..*****..

Mafundi wetu wajenge utamaduni wa specialisation...
Kwa mfano fundi garage yenye mafundi kumi, inapendeza kika mmoja awe hodari wa mfumo fulani kama walivyo madaktari..

Yaani fundi wa Suspension abobee huko

Fundi wa brake abobee huko..

Fundi wa Cooling system abobee huko...

Hali kadhalika fundi engine, geabox,music na kadhalika...

Tamaa za mafundi ndiyo zinafanya wanamnunulisha mteja spea ambazo fundi hana uzoefu na mfumo husika..

shubamiti ..
 
Nakubaliana na wewe..
 
Rav 4 kilitime inagonga, miguu ya mbele nimebadilisha shockup na stablizer link lakini bado inagonga, naombeni msaada wadau tatizo ni nini?
Shock up zikichoka gari haigongi gongi...bali huwa zinakita ukipiga kashimo au kabump...utasikia zinakita khuu!!
.
Kugonga gonga kagua
Ball joint, stabilizer bars/link, bush za wishbone, juu kabisa kwenye shock up inapoungana na body kuna bush flani inaitwa topedi(sijui spelling sahihi), mfumo wa usukani nk...
Hapa unatakiwa umpate fundi anayeielewa kazi yake na anayejua mfumo mzima wa Suspension unavyofanya kazi....vinginevyo utanunulishwa spea nyingi sana mwisho wa siku unakuta ni ball joint tu..
 
Fundi anayejielewa ugonjwa wa kugonga gonga miguu wala si tatizo kwake...kwa sababu akijaribu tu kuendesha gari lazima atahundua kinachogonga ni nini...
Na isitoshe mafundi ni wavivu....
Fundi anayejali kazi yake angefungua suspensions parts moja baada ya nyingine na kuikagua kwa weledi, hapo lazima kifaa kibovu kingepatikana....

sasa fundi vilaza wanakariri kuwa gari likigonga miguu basi ni shockup
 


Kuna muda huwa natamani ningekuwa fundi gari na niwe muaminifu, nachaji ufundi bei ya kawaida kulingana na tatizo la gari, Ila likitoka hapo mteja anaona tofauti. Nina uhakika ningekuwa naingiza hela hadi nazikimbia maana wako watu na magari yao na pesa wanazo wanachohitaji ni huduma bora....

Well soon nastaafu, nikituliza akili yangu kwenye ufundi nna uhakika kuna wataotoka mikoa mbalimbali kufata huduma au ufundi wa gari.

Alnuru.
 
Umeangalia Ball Joints na Tie rod ends Mkuu??
Kuna siku nikienda garage nikatajiwa hivyo vitu.....nikachanganyikiwa vipe fundi alitawanyisha hizo kitu kwenye tairi zote mbili....uzur wa toyota sasa kufika nikaambiwa 125K kinatoa kama nimeambiwa buku 10K vile.... Toyota hoyeeeee......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…