Ray C afungua mlango kwa Mwanaume yeyote anayetaka kumuoa

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Msanii wa muziki Rehema Chalamila aka Ray C amefungua mlango kwa mwanaume yoyote anayetaka kumuoa ajitokeze ilimradi awe na vigezo 10 ambavyo ameviainisha. Kupitia ukurasa wake wa instagram Ray C ameandika:

Rehema Chalamila ‘Ray C'

"Habari zenu wapendwa wote dunia nzima!Leo na habari nzuri sana kwenu,Naomba kuwatangazia kuwa natafuta Mchumba wa kuishi nae milele! nataka niwe nae milele na nimzalie watoto wawili wa kike na wakiume!!!!

Ila naomba niwambie kabisa masharti;

1.Awe mpole ili nikikasirika anibembeleze

2.Awe anapenda muvi za kihindi ili nikiwa na stress aniwekee nyimbo za kihindi maana ndio raha ya moyo wangu.

3.Asiwe muongeaji sana sababu huwa sipendi makelele.

4 Anipende na ubonge wangu huu asije akaanza kunambia baby anza mazoezi au dah baby zamani ulikuwa bomba au rudisha kiuno hapo hatutaelewana.

5.Awe ananipikia nikichoka maana navutiwa nikimuona mwanaume anapika.

6.Awe na Mimi muda wote maana na wivu sana ikiwezekana tufanye kazi ofisi moja au awe ofisi ijengwe hapo hapo nyumbani.

7.Awe mvumilivu maana nikiwa na hasira huwa naongea kwa sauti ya juu sana.

Rehema Chalamila ‘Ray C'

8.Asiwe na rafiki wengi,na akitaka kuonana nae na mi niwepo maana si mnajua wanaume tena wakikutana huwa wanashaurina mabaya.

9.Awe anajua nyimbo zangu zote ndio ntaamini kweli ananipenda.

10.Sharti la mwisho kabisa ambalo ni muhimu sana kwangu ni hili tuwe tunatumia simu moja na Namba moja, maana kanisani tunafundishwa kuwa ndoa maana yake tumeungana na kuwa kitu kimoja kwahiyo kama mume na mke tunalala pamoja kitanda kimoja na kuishi pamoja kwanini tusitumie simu moja!Sioni tatizo!

Kama una ndugu,jamaa.kaka,rafiki yuko single basi mjulishe tangazo hili huezi jua unaeza ukashangaa nimekuwa shemeji yako au wifi yako".
 

Attachments

  • RayC.jpg
    18 KB · Views: 31,141
hata bureeeee simuoiiii...
 
Mh". Wengine mnaponda tu ila moyoni mnalo.
 
Kwanza lazima ajue kuwa yeye wala sio Ray c tena yeye ni Rehema tu wala hana la zaidi.

Pili hayo masharti aliyopanga ni kwa vigezo vipi kwa mfano? Akumbuke hata dozi ya metho hajamaliza....
Kama vile haitoshi kwa mkorogo huo hivi kuna mtu atashawishika kweli???

Wanaume kazi kwenu
 
hahahahahahaaaaaaa aseeeee, ndo wanawake wetu hawa. miaka 15 mpaka ishirini wanaringa mbayaaaaa, 20 mpaka 28 mcharukoooooo hatareeeeeee anajua leo nikiachana na huyu kuna jamaa linatia team sasa hv ye hana shidah.......
30 na kuendelea anaanza kusaka mume ati ...... waru washa lina asali unakuja na mzinga mkavu.... mweeeeeeeh..
Apige moyo konde kuna madingi yanahitaji mke dizain yake.....
cha kumshauri , kwa ndoa za kanisani haipati ng'oooooooo
aslim tu huyu dada waislam wafanye nusra aseeeee
 
Mnavyo mkataa .duh! nahisi anajisikia vibaya sana .khaaa khaaaaa teh teh kwi kwi teh teh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…