Ray C ala tenda nono hospital ya Mwananyamala

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Baada ya kupitia kipindi kigumu cha kutumia madawa ya kulevya ' unga ' kisha kunusuriwa, super lady kwenye Bongo Fleva , Rehema Chalamila ' Ray C ' , hatimaye mambo yameanza kumnyookea baada ya kulamba shavu tenda nono ya kulisha Hospitali ya Mwananyamala , Dar .

Super lady kwenye Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C '.

Kwa mujibu wa chanzo makini cha Ijumaa Wikienda, Ray C almaarufu Kiuno Bila Mfupa amefungua bonge la ' restauranti' maeneo ya Mwananyamala Hospital, ambapo amepata tenda ya kuwahudumia chakula wafanyakazi wa hospitali hiyo na Idara ya Maji ( Dawasa ) ambapo anafanya kazi hiyo kwa saa ishirini na nne na muda mwingi anakuwepo yeye mwenyewe.

"Bidada sasa hivi yupo njema sana. Kalamba shavu la kulisha Hospitali ya Mwananyamala na Dawasa na hapo ni mchana na usiku so yupo bize kinoma.

Baada ya kunyetishiwa ishu hiyo, wanahabari wetu waliusaka mgahawa huo na kufanikiwa kuupata ambapo walimkuta Ray C akiwa bize kuhudumia wateja ambapo alisema:

"Namshukuru Mungu kwani nimepata tenda ya kuwapikia chakula wafanyakazi wa Mwananyamala na wale wagonjwa ambao ni waathirika wa madawa ya kulevya. "
 

Attachments

  • 1410152947455.jpg
    59.4 KB · Views: 1,278
Mmh unakumbuka shuka wakat kumeshakucha, usije tu ukawa unafanya biashar ya kuuza viungo vya binadamu apo mwana nyamal, maana nyie wasanii hamuaminik kwa biashara haramu tu hamjambo
 
Heaven on Earth siku izi huonekani wenzetu kumbe mmepata tends nono mwananyamal, hongeren bhana, mida ya mchana nitapita apo kupata lunch na kufuata umbea najua nitapata mawil matatu apo
 
Last edited by a moderator:
Ni vizuri binadamu ukikosea ktk maisha unarekebisha na maisha yanasonga mbele, aangalie mbele sababu ya kale yamepita amekuwa Ray C mpya.
 
Safi sana. Ni practical success wale walioacha madawa. Na wale wanaoendelea na madawa Mungu akutane nao wabadilike kupitia Rehema Chalamila.
 
Out of topic ::HAPPY BIRTHDAY WARUMI,LEO NI SIKU YAKO YA NZURI YA KUZALIWA,BASI BINAMU warumi NAKUTAKIA FURAHA NJEMA YA KUZALIWA KWAKO😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀happy birthday my cousin
 
Last edited by a moderator:

Ahsante binamu, nimefuraijeee, leo ndo nazaliwa binamu aiseeh, happy birthday to me
 
Last edited by a moderator:
Nafurahi Sana nikiskia positive things kutoka kwa wasanii wetu
 
Aisee happy birthday cousin warumi. Mungu akupe maisha marefu yenye utimilifu
 
Last edited by a moderator:
Ooh,happy birthday Mr.gossip warumi....I guess u have 25-29 yrs...huvuki hapo
 
Happy birthday warumi long live endelea kutupa info
 
Last edited by a moderator:
Ooh,happy birthday Mr.gossip warumi....I guess u have 25-29 yrs...huvuki hapo

Aahah ahaha, kwa nn? Kwa taarifa yako nina miaka 32 mwenzio ooh shaur zako, thanks for the wishes
 
Hongera tutajie jina la hiyo restaurant
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…