RAY C Ampa Nora kichapo

RAY C Ampa Nora kichapo

Binti Magufuli

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2011
Posts
7,479
Reaction score
5,157
[h=3]RAY C AMPA KIPIGO NORA[/h]Posted by GLOBAL on October 28, 2013 at 8:00am1 Comment 0 Likes
Na Musa Mateja

KATIKA hali ya kushangaza, siku chache baada ya kuripotiwa kupona na kuacha matumizi ya madawa ya kulevya, mwanamuziki Rehema Chalamila ‘Ray C’ anadaiwa kugeuka mwanamasumbwi na kumpa kipigo mwigizaji Nuru Nassoro ‘Nora’, Ijumaa Wikienda limenyetishiwa.
Rehema Chalamila ‘Ray C’.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo lilijiri wiki iliyopita ndani ya studio moja ya kurekodia muziki iliyopo Kinondoni, Dar ambapo wawili hao walikutana walipokwenda kurekodi ngoma zao.

Ilidaiwa kuwa akiwa studio hapo,…
http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/ray-c-ampa-kipigo-noraNa Musa Mateja
KATIKA hali ya kushangaza, siku chache baada ya kuripotiwa kupona na kuacha matumizi ya madawa ya kulevya, mwanamuziki Rehema Chalamila ‘Ray C’ anadaiwa kugeuka mwanamasumbwi na kumpa kipigo mwigizaji Nuru Nassoro ‘Nora’, Ijumaa Wikienda limenyetishiwa.
Rehema Chalamila ‘Ray C’.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo lilijiri wiki iliyopita ndani ya studio moja ya kurekodia muziki iliyopo Kinondoni, Dar ambapo wawili hao walikutana walipokwenda kurekodi ngoma zao.
Ilidaiwa kuwa akiwa studio hapo, Nora alikutana na Ray C ambaye pia alizama mahali hapo bila mawasiliano na prodyuza anayemtengenezea ngoma mpya.
Chanzo hicho kilipasha kuwa baada ya Ray C kuingia studio hapo alimkuta prodyuza huyo akiandaa ngoma ya Nora ambapo alihoji kilichompeleka mwigizaji huyo mahali hapo.
Rehema Chalamila ‘Ray C’.
Ilidaiwa kuwa prodyuza huyo ambaye jina halikupatikana alimwambia Ray C kuwa Nora alifika kurekodi wimbo wake.
Ilisemekana kuwa Ray C hakuridhishwa na majibu hayo, akaomba asikilizishwe ngoma hiyo ya Nora lakini baada ya kusikiliza ilidaiwa kwamba Ray C aliiponda mbele ya Nora, jambo ambalo mwigizaji huyo hakufurahishwa nalo.
Ilidaiwa kuwa Nora alipandwa hasira na kujikuta akimjibu mbovu Ray C.
Habari ziliendelea kutiririka kuwa siku hiyo walimalizana kwa kusonyana na siku iliyofuta walikutana tena studio hapo ambapo Ray C alidaiwa kutinga akiwa ‘masanga’.
Ilisemekana kuwa alipomuona Nora alianza kumpa vijembe, jambo lililosababisha Nora kushikwa hasira ndipo wakavaana na kuzichapa.
Hata hivyo, ilidaiwa kuwa Ray C ndiye aliyeibuka bingwa wa ndondi hizo kwa kumtwanga Nora hadi kumvimbisha jicho kabla ya maprodyuza na watu wengine kufanya kazi ya ziada kuwaamulia.
Ilisemekana kuwa baadaye Ray C alitolewa nje ndipo akahamishia hasira kwenye gari la Nora aina ya Toyota Vitz kisha akalivunja kioo na kutambaa zake.
Baada ya kupenyezewa ‘niuz’ hizo gazeti hili lilimtafuta Nora ambaye alikiri kutokea kwa sekeseke hilo huku akibainisha namna alivyoumizwa jicho lake na kuvunjiwa kioo cha pembeni cha gari lake.
Aliongeza kuwa siku hiyo alipoteza pochi wakati wa ugovi huo.
“Ray C alinikuta studio nikifanya wimbo, kilichonishangaza baada ya kuniona tu alibadilika ghafla.
“Nilijua angenishauri kwa kuwa ndiyo ninaanza gemu kumbe mwenzangu alifikiria vingine,” alisema Nora na kuongeza:
“Mbali na kuniumiza jicho lakini alinifanyia mambo ya ajabu sana, kama kusingekuwa na watu wa kutuamulia basi chochote kingetokea.
“Sikwenda kuripoti polisi. Niliamua kusamehe kwa sababu kuna watu walinisihi niachane naye kwa sababu bado kuna mambo yanamwendesha.
Kwa upande wake Ray C alitafutwa kwa kila njia kupitia simu ya mkononi na kumvizia studio lakini hakupatikana hivyo juhudi za kumpata zinaendelea.

Mhh huyu ray C anatafuta kick za lazima ili arudi tena! Na hayo mapoda sijui bado hayajatoka kichwan
 
Nora naye anataka kuimba? Snura anawadanganya wenzake kua wanajua kuimba au!
Au ray c amesikia rugay kamchumisha mboga nora!
 
Daaa Mrembo by Nature umesahau kuwa rayc anaumwa?

Huyu rayc naona anataka kurudi kwenye fan.
 
Last edited by a moderator:
hahahahahahaaaaa. bongo yetu hii..
 
Duh kila atakachofany itaonekana ni bhang hat kama yu mzima,pole sana najua inauma
 
hee bongo muvi wote wanahamia kuimba?kweli muziki wa kitanzania umekuwa rahisi sana
 
nadhani ray c bado ana chembechembe kwenye ubongo
 
muziki unalipa kuliko movie au.......ila.kuimba kuna wenyewe jamani
 
Nora naye anataka kuimba? Snura anawadanganya wenzake kua wanajua kuimba au!
Au ray c amesikia rugay kamchumisha mboga nora!

Huyu m.she.nzi boss wa THT aliposikia m-nako Eyez anakula huyo ray c akawawekea kauzibe na kumnunua ibra had nako ikavunjika na kusababisha album yao ya hawahemi street husle vol.1 isiende sokoni. Ndo akasabaisha kufa kwa mapinduz ya hip hop bongo! Walivyopotea wote kwa poda ndo akatokeza kuwasaidia na kuwapa promo uchwara!

Hahaha kuwa msanii bongo lazima uwe "'msanii"
 
Haya mchuga.
 
ila ray c amesaidia kuchuja msanii uchwara,et nora nae anaimba mmmhh....wangekuwa wanachujana hv ingependeza sana
 
nora nae mwanamuziki!! kazi ipo.
 
bongo flava ni kichwa cha mwendawazimu.Hakuna aliyekwenda bongo flava kashindwa kabisa.nashangaa mtu anajiita star wa bongo flava.Kaweza bibi Cheka nani atashindwa.
 
Back
Top Bottom