Ray C: 'Dawa za kulevya ni hatari'

engmtolera

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
5,149
Reaction score
1,441
Katika Misemo ya kale upo msemo usemao aisifuye mvua,imemnyea.

Usemi huu unaweza kufananishwa na kauli ya Msanii maarufu wa Muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Rehema Chalamila almaaruf Ray C, ambaye hivi karibuni alitoa wito kwa serikali kuwanyonga wale wote wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Mwanamuziki huyo hivi sasa yuko kwenye kliniki maalum akipata tiba kutokana na kuathiriwa na matumizi makubwa ya dawa za Kulevya, baada ya kupata msaada kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania.

Erick David Nampesya alikutana naye hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Chanzo:Ray C: 'Dawa za kulevya ni hatari' - BBC Swahili - Medianuai
 
Mkuu kuna mahali nilisoma kwamba tayari ameanzisha asasi ya kuelimisha vijana maadhara ya dawa za kulevya. Huenda akawa balozi mzuri wa kupambana na matumizi ya dawa hizi ila nayo ni safari ndefu kwake kwani mtandao wa madawa ya kuelevya ni mkubwa na una nguvu na ndio maana hata umeshindikana kutokomezwa duniani kote. Labda tusubiri baada ya kukamatwa kwa Guzman kama kutapunguza huo mtandao.
 

ni kweli
anadai tuisubiri ipo njiani yaja na mwezi wa 3 anategemea kuanza kutoa ngoma zake,hizi ni habari nilizosikiliza kutoka BBC SWAHILI,
nadhani hatarudia tena kunusa sembe,maana amepata fundisho kwa kweli
 
Ye afanye yake atoe elimu kwa mateja wenzie swala la kunyongwa ye mbona hajanyongwa
akwende zake alilazimishwa
 
Ye afanye yake atoe elimu kwa mateja wenzie swala la kunyongwa ye mbona hajanyongwa
akwende zake alilazimishwa

Anafanya yake na haya ni maoni yake yanaweza kufuatwa ama la.si lazima yafuatwe.
 
Akajaribu bongo movie maana music hana jipya tena mvuto hanaa..
 
Eti baada ya yeye kupona tena kwa kutibiwa na ------
ndo anatoa maoni watu wanyongwe
mi naona anyongwe yeye kwanza
na atakuwa hajapona huyo

Alikuwa anajifanya eti ana hasira nao sana , angenyongwa yeye kwanza tipwa tipwa mwil umejaa madawa ya kulevya..
 
Eti baada ya yeye kupona tena kwa kutibiwa na ------
ndo anatoa maoni watu wanyongwe
mi naona anyongwe yeye kwanza
na atakuwa hajapona huyo

kwa hiyo unawaunga mkono wauza unga? maana wanakuona humu JF,watakutafuta uwabebee mzigo kwenda China,then unapotea JF na bongo kwa ujumla na sisi kazi yetu ni kusema R.I.P
 
Akakae na Ruge huko mxxxxiiiuuy!!
 
kwa hiyo unawaunga mkono wauza unga? maana wanakuona humu JF,watakutafuta uwabebee mzigo kwenda China,then unapotea JF na bongo kwa ujumla na sisi kazi yetu ni kusema R.I.P

R.i.p ni haki ya kila mtu sio wauza sembe tu...
kwani unajuaje sibebi?
 
he he he nicheke mie
weekend njema engineer.

tunawategemea jamani,taifa hili lenu,nyie ndio nguvu kazi ya hii nchi jamani,sie tumeshazeeka hivyooooooooooo.
Weka mbali na watoto-dawa za kulevya zinauwa
hahahahahahahahahahahahahaha
 
tunawategemea jamani,taifa hili lenu,nyie ndio nguvu kazi ya hii nchi jamani,sie tumeshazeeka hivyooooooooooo.
Weka mbali na watoto-dawa za kulevya zinauwa
hahahahahahahahahahahahahaha

we ushazitafuta hadi umezeeka
acha nami nitafute ningali kijanaaaaaaaaaaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…