Ray c katisha jamani anastahili pongezi hembu soma hapa :

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
[h=3][/h]

Mwaka 2013 umekuwa wa mafanikio makubwa kwa Rehema Chalamila aka Ray C. Kubwa anamloshukuru Mungu ni kuokolewa kutoka kwenye maangamizi yaliyosababishwa na kuathirika na matumizi ya madawa ya kulevya, thanks kwa Rais Jakaya Kikwete aliyeamua kugharamikia matibabu yake. Baada ya matibabu hayo, muimbaji huyo wa ‘Niwe Nawe Milele’ amerejea kwenye afya yake ya kawaida na sasa yupo busy kurekodi nyimbo mpya na huenda mapema mwaka 2014 akarejea kwa kishindo. Pamoja na kupewa gari nzuri ya kutembelea, Ray C ameionyesha nyumba yaka anayoijenga na iliyokamilika kwa asilimia kubwa huku ikifanyiwa upambaji wa ndani tu. Ray C ameionesha nyumba yake kwenye Instagram kwa kuandika: Love the color of ma new house!!!! Under construction #godisgood#workhardplayhard."
 
naomba kujua anajishughulisha na nini kinachomuingzia kipato adi anakua na jeuri kiasi hiki...
Ni mwanaume au?
 
naomba kujua anajishughulisha na nini kinachomuingzia kipato adi anakua na jeuri kiasi hiki...
Ni mwanaume au?

Ukisoma hapo utaona ata gari amepewa. Nyumba yake aliuza ili anunue madawa.

Kuna mtu nyuma yake
 
kweli niamini usishindane na mwanamke kesho atahongwa noah
 
Mambo ya Promoter bonger aka Yahya or Mheshimiwa fulani🙊🙊🙊🙊
 
Kahongwaa tu huyo atuambie na shughuli anayofanyaa ndio hivyo anatumia fursaa
 
Kahongwaa tu huyo atuambie na shughuli anayofanyaa ndio hivyo anatumia fursaa
Hivi hata hao wahongaji nao wanamuonaga huyohuyo tu,mbona wamejaa wasichana wengi tu na staha zao lakini hawawapati..??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…