Ray: Chuchu ndo kila kitu kwangu

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
LEGENDARY kwenye anga la sanaa Bongo, Vincent Kigosi ‘ Ray ’ kwa mara ya kwanza amefunguka kuwa mpenzi wake wa sasa , Chuchu Hans ndiye kila kitu na kilichobaki ni ndoa tu .

Akizungumza na paparazi wetu, Ray alisema licha ya kupitia katika changamoto nyingi za mapenzi lakini kwa Chuchu amefika na haoni tabu kujinadi kwa mtu yeyote juu ya penzi lake hilo.

“Chuchu ndiye kila kitu kwangu , tunaendana kwa kila kitu hivyo nitakaowaudhi kwa kumpenda yeye, wanisamehe , ” alisema Ray .

Ray kabla ya kuwa na Chuchu, kwa nyakati tofauti alikuwa akitajwa kushea penzi la mwigizaji Ruth Suka ‘ Mainda ’ na Blandina Chagula ‘ Johari’ .
 
Attachments

  • 1416689642012.jpg
    39.3 KB · Views: 2,040
afadhali mi nimemkubali ray kwa kuamua kuweka wazi uhusiano wake na chuchu hongera sana maana kungine watu walikua wanahisi tu hongera kigosi
 
Yani ulipomtaja mainda suka nikamkumbuka Max wa zembwela,kusalimika ni ngumu kama hamtoacha zinaa,gonjwa limekaa pabaya mtandao ni mpana sana.

Mkuu umefunguka vizuri sana..hata huyu Ray mwenyewe..mmh..sijui maana kuna sehemu moja nlimuona..hatari sana..
 
Huyu nilianza kumuona Boya baada ya Kujichubua.
 
Eee mnasemaga hivyo hivyo baada ya muda utasikia hakukidhi viwango tumeamua kumpumzishanaa
 
afadhali mi nimemkubali ray kwa kuamua kuweka wazi uhusiano wake na chuchu hongera sana maana kungine watu walikua wanahisi tu hongera kigosi

Nilijua tu lazima ushangilie...khaaa
 
Yani ulipomtaja mainda suka nikamkumbuka Max wa zembwela,kusalimika ni ngumu kama hamtoacha zinaa,gonjwa limekaa pabaya mtandao ni mpana sana.

Ray,johar na mainda mbona wa siku nyingi, bora mwenzao mainda kajisalimisha kwa yesu, ila wengine hao bado wanakula ujana, washasahau dozi
 
Eee mnasemaga hivyo hivyo baada ya muda utasikia hakukidhi viwango tumeamua kumpumzishanaa

Wanavyojitahidi kupaisha mahusiano yao sasa, sema wana gundu watu ata hawawafuatilii sana mamayo zao watajitangaza sana
 
toka afe the great,ray hasikiki kabisa mpaka ameamua kuanza drama kama za mama ubaya
 
Ray,johar na mainda mbona wa siku nyingi, bora mwenzao mainda kajisalimisha kwa yesu, ila wengine hao bado wanakula ujana, washasahau dozi

TACAIDS wakiendelea kula hela bila kufanya kazi,baada ya miaka kadhaa 20 ijayo tutakuwa kama Botswana.
 
Siku ya siku vifua vinaanza kuwasumbua maana kama alitoka kwa mainda ila mhhhh!!!!
 
mapenzi haya ya uswahilini na karne hii na fani yenyewe ya kuigiza! maskhara hayo lakini wakimwagana bila hata ya promo tutajua tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…