Rayuu: msanii wa Bongo Movie na sakata la kutoka na mume wa mtu

Rayuu: msanii wa Bongo Movie na sakata la kutoka na mume wa mtu

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304
Rayuuuu.jpg

MSANII wa filamu na tamthilia bongo Rayuu, inadaiwa kuwa amenusurika kupelekwa polisi na mwanamke mmoja kwa madai kuwa alikuwa akitembea na mume wake, huku pesa nyingi za matumizi zilikuwa zikienda kwa msanii huyo.

Wiki iliyopita hali ilikuwa ngumu kwa msanii huyo kwani taarifa za kupelekwa polisi zilimpa wakati mgumu hadi kuchukua hatua ya kujifungia ndani ili kupumzika na kupisha taarifa hizo ambazo zingemchafua pengine hata kujiigiza kwenye matatizo makubwa.

Chanzo kimoja kilichozungumza na mwandishi wa DarTalk awali kabisa kilidai kuwa msanii huyo alikuwa akitembea na jamaa huyo bila kujua ni mume wa mtu huku wakitanua sehemu tofauti tofauti za starehe.

Hata hivyo taarifa hizo za kuonekana sehemu kadhaa na jamaa zilimfikia mke huyo anayedaiwa kuwa mke wa jamaa, ndipo alipotafuta namba ya simu ya Rayuu na kumtaka aachane na mume wake mara moja bila hivyo anaweza kumfikisha kituo cha polisi na akajibu mashtaka.

“Wiki iliyopita tu huyo mwanamke baada ya kupewa taarifa kuwa mume wake anakula bata na msanii huyo, ndipo alipoamua kuchukua maamuzi ya kumpigia simu Rayuu ili kumwambia achane na mume wake,” kilisema chanzo hicho.

Hata hivyo mwandishi wa DarTalk bila kusita alimtafuta Rayuu ili kuzungumzia ishu hiyo, ambapo alidai kuwa alipigiwa simu na mwanamke huyo ya kumtaka achane na mume wake, lakini awali kabisa hakujua kama ni mume wa mtu.

Alisema hakuwa na makosa kwani jamaa alipomfuata hakusema kuwa ni mume wa mtu na wala hakuwa na ishara zozote zinazoonesha ana mke nyumbani na muda wote alipomtafuta walikuwa wakionana na kufanya yote kama wapenzi.

“Sikujua kama ni mume wa mtu na nimekuwa naye katika mahusiano kwa muda mrefu lakini nilipatwa na mshtuko baada ya mwanamke anayedaiwa kuwa mke wa jamaa huyo kunipigiwa simu tena kwa matusi na kudai kuwa nikae mbali na mume sikujua anazungumzia nini lakini baada ya muda jamaa mwenyewe akaniweka wazi kuwa ni mume wa mtu,” alisema Rayuu.

Alipoulizwa swali kuwa baada ya kujua jamaa ni mume wa mtu alichukua hatua gani, alidai kuwa hakuwa na kitu cha kufanya zaidi ya kuachana na jamaa kwani hataki yaje kumkuta makubwa zaidi.
 
Ila jina lako halifananii hii habari,inatia ukakasi sababu uyu rayuu ni nan?ana tax identification number? Si ajabu hakatwi kodi yoyote na serikali as anategemea wanaume wamuhonge,amefanya nini sababu naangaliaga bongo movie ata simjui au kama ndo anatafuta skendo ili auze kama alivyoanzaga anti ezeki...otherwise hii abari ni maisha yake binafsi wala hana umaarufu wowote labda kama ni yeye ameanzisha hii thread.
 
hivyo vinyota hapo ndio copy and paste tonto dikeh??? kazi wanayo!
 
Ila jina lako halifananii hii habari,inatia ukakasi sababu uyu rayuu ni nan?ana tax identification number? Si ajabu hakatwi kodi yoyote na serikali as anategemea wanaume wamuhonge,amefanya nini sababu naangaliaga bongo movie ata simjui au kama ndo anatafuta skendo ili auze kama alivyoanzaga anti ezeki...otherwise hii abari ni maisha yake binafsi wala hana umaarufu wowote labda kama ni yeye ameanzisha hii thread.

tayari ana skendo aliwai piga uchi ili kuonyesha tatuu yake,akafukuzwa kwao akaenda kuishi kwa mr chuzi,watu wana haki ya kujua mambo wanayoanya wasanii wa bongo na maisha yao kwa ujumla,na watu watajifunza kutoka na makosa wanayofanya awa wanaoitwa kioo cha jamii,awa wasanii wanachangia mambo mengi ikiwa kwenye kuharibu au kurekebisha jamii,hivo habari zao lazima zitolewe zikiwa mbaya au nzuri
 
Mbona akienda polisi atajichora. Kwa sababu kesi za ugoni si jinai. Ni za madai.
 
Hah hah haah jana aliniambia ''kwa kibongo bongo hao ni macerebrity, tutake tusitake''

bongo hakuna macelebrities,kuna wasanii uchwara tu,sasa nyie mnataka tuweke habari zakina beyonce,50 cent tu,tunakomaa nao awa awa wa nyumban,bongo kama kuna macelebrities basi ni kidogo sana
 
hivi siku hizi hii ni storry tena si sifa...na wanatambiana kwa hilo.
 
Back
Top Bottom