<div class="bbWrapper"></div>
- Tunachokijua
- Madai ya kuwa msanii Raymond Shaban Mwakyusa maarufu kama Rayvanny kumpeleka msanii aliyekuwa akimsimamia Nassib Abdul (Diamond) yalizuka punde tu baada ya kuondoka katika label ya WCB na kuhamia katika label yake ya Next Level Music (NLM) katika Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA).
Baadhi ya tetesi zinadai kuwa msanii huyo amempeleka Diamond BASATA kwa madai yanayotokana na baadhi ya matukio likiwemo la kupata jina ndani ya WCB hivyo kama ameamua kujitenga ni lazima alipie gharama kwa kuvunja mikataba ya kikazi inayowaongoza jambo lililopelekea kwa madai ya tetesi kuandikiwa kulipa kiasi cha shilingi za kitanzania 800,000,000/= kama fidia.
Katika kuthibitisha madai hayo vyombo vya habari mbalimbali vimejaribu kufuatilia madai hayo ya BASATA na kuonesha ni kweli walionekana katika eneo la BASATA 27/ 07/2022 hilo lakini hakukuwa na Ushahidi unaoonesha kuwa walienda kwa sababu ya madai hayo kulingana na jambo hilo kutokuwekwa hadharani