Rayvanny; Nitaondoka WASAFI (WCB) kwa amani

Kiukweli wasanii ambao diamond alibahatisha ni Kondeboy , ray vanny na Zuchu , Mboso still anasua sua japo ni afadhali , lava lava ni gharasa , qeen darling ndo usiseme[emoji3][emoji3]
Mbosso huyu huyu au yupi asee?
 
Ndani ya Wcb msanii mwenye pesa ni boss wao tu. Wengine wanaambulia umaarufu tu. Ukiwa chawa tu wa Wcb lazima uwe maarufu sembuse msanii mkwanja wako sawa na wakina gigy money .
Vipi label nyingine kama Konde Gang,Kings kuna msanii mwenye hela kuzidi Boss wake au kuzidi wasanii wa WCB?
 
Mondi Hana Kolabo nyingi sababu nyimbo zake hazipigwi na hizo media?

😂😂😂😂

Kipindi ambacho ana mgogoro na hizo media kishafanya Kolabo na Alicia keys,Omarion na kama hujui Jeje ina rmx yake kamshirikisha Tyga vilevile na Rema.Kama hujui tokea Diamond ache kupigwa na hizo media ndio amekua akipata show nyingi,yaani mpaka sasa diamond kishapiga show 95% ya nchi za Sub Saharan Africa.

Kuna kipindi ilikuwa ukipiga show Wasafi basi sahau kupata show kwenye matamasha yanayo anadaliwa na hizo radio nyingine tatu hata Airtime hupati ,hili aliliongelea Linah kipindi akihojiwa na Dizzim.

Kwa hiyo wewe ulitaka Mondi anyimwe airtime hili afe kimziki?Kama hujui Diamond alihisi hili tokea kipindi kile cha Kili music awards,akainvest kwenye social media na ndizo zilizo mbeba 2017-2018 ali survive bila Clouds,EATV na EFM.

Halafu jiulize source ya kwanini Mondi hana mahusiano mazuri na hizo media?

Halafu ujiulize tena kwanini baadhi ya wasanii (Wagosi,Suma G,Rama dee) waliacha muziki sababu ya hizo media?

Unasema Mondi ana roho mbaya vipi na hizi media zilizo ua vipaji vya watu kwa makusudi,hawa nao wana roho nzuri?
 
Mbona mpaka sasa hawajapotea kwenye Digital Platforms (YouTube,Boombplay,AudioMack) wametawala wao.
 
Boss wa WCB hataki kumaliza bifu na hizi media kubwa...
Anajua kabisa ngoma zao ziki achiwa zipigwe kwingine media yake itayumba hato pata wasikilizaji...
Boss hataki kumaliza beef au hizo media ndio hazitaki.Nikwambie kitu nina uhakika hata beef likisha WCB itazidi kuwa juu sana,sababu itakuwa uwanja mkubwa ktk burudani na radio ndio itazidi kuwa kubwa.
 
Kwa Yale aliyoyapitia Mond ni mwehu Tu anayeweza kumuona hafai , tena mtu kama harmonize alitakiwa awe na heshima ya Hali ya juu Sana Kwa Mond , Diamond kapambana vita vikali Sana mpak kufika hapo alipo na crew yake , amemvusha harmonize katika dimbwi zito la matope hadi kumng'arisha kama dhahabu Safi , inashangaza Sana anapoonyesha dharau ambazo hazina msingi ..... Wakat fulan Diamond alihojiwa na kudai kuwa kuna watz wenye nguvu walimuwekea kiwingu kizito nyimbo zake zisipigwe MTV , Kwa juhudi akaamua kupitia Nigeria , ...... Katika industry ya mziki huyu mwamba ni mwanaume wa Karne ......
 
Mbona mpaka sasa hawajapotea kwenye Digital Platforms (YouTube,Boombplay,AudioMack) wametawala wao.
Mkuu huko vijijini watu hawajui kuhusu boomplay, Digital sijui oudiomark, wao wanasikiliza radio na kutizama TV
 
Kwakifupi Media yake imembeba kimtindo pia tofauti na wasanii waliokua wanategemea media za watu ndiyo walipotea baada ya kutocheza ngoma zao

Kiufupi Mondi alishajua wanataka kumpoteza kwenye game ikabidi achanue mbawa ili apae angani kabisa na amefanikiwa kimtindo.
 
Mkuu huko vijijini watu hawajui kuhusu boomplay, Digital sijui oudiomark, wao wanasikiliza radio na kutizama TV
Ndipo dunia inapo elekea,wewe ukitaka kukomaa na vijini sawa ila nijuavyo mimi vijini watasikia kwenye maradio,Tanzania kuna radio zaidi ya 128 so watasikia.

Ila Digital platforms ndio future biashara ipo huko,siku hizi hata ukubwa wa msanii unapimwa kwa kuangalia mauzo na streaming kutoka huko.
 
Sio kimtindo Diamond kafanikiwa sana,Diamond ana vision na ndio maana kipindi kile cha Kili Awards 2014,alikimbilia kwenye Digital Platforms aliiona kesho kupitia hizi digital platforms na ndizo zinampa show kama utitiri,kupiga show zaidi ya 95% za nchi ktk ukanda wa Sub Saharan ni rekodi ya kutisha na hizi show zote zimefanyika viwanjani na kwenye venue zenye kuingiza watu wengi.

Alafu ni kwambie kitu Diamond hajasoma ila anajua kuwatumia watu waliosoma ndio maana kwa kujua umuhimu wa Digital Platform Diamond ana watu special kwa ajili ya kufuatilia na promotion kazi zake na Label yake kwenye Digital Platform.
 
Ila upande mwingine inabidi ashukuru media kwa kumbania kwani zimemchallenge sana bila media kumbania huenda angejisahau na isingekuwepo wasafi fm na wasafi tv

Ila yote na yote nimpongeze kwa hatua aliyofikia.
 
Kwamba atakufa kimuziki?
 
Kwamba atakufa kimuziki?
Wewe unaonaje.

Stori zilizopo jamaa Hana mpango wa kulipa hata 100.

Digital platforms zote Bado wanashikiria Wasafi. Amebaki na Shows tu.

Unafanya Shows unapata pesa, unatengeneza video na audio unawapelekea Wasafi wakuwekee kwenye digital platforms halafu Ngoma zinauzwa wanachukua mgawo wao, na Bado Ngoma zote siyo Mali yako.
 
Sio ndio mkataba unavyosema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…