Rayvanny wa WCB kuwasili nchini leo; Kumbe hakuwaaga Basata?

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532


Msanii wa kizazi kipya, Rayvanny aliyeshinda tuzo ya BET kipengele cha International Viewers Act 2017, atawasili nchini leo saa 8 mchana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)

Rayvanny alipata tuzo hiyo nchini Marekani Juni 25 na kuwa msanii wa kwanza kushinda tuzo hizo kubwa.
Rayvanny ameambatana na Babutale ambaye ni mmoja wa mameneja wa Kundi la WCB.

Meneja wake, Makame Fumbwe amesema, Rayvanny atakapowasili, msafara wake utatoka JNIA na kupita katika mitaa mbalimbali ya jiji na baadaye atakwenda katika mahojiano kwenye kituo cha Clouds.

Katibu Mkuu wa Basata, Godfrey Mngereza licha ya kumpongeza kwa mafanikio hayo lakini amesema Rayvanny hakutoa taarifa kwa baraza kuwa anakwenda kwenye tukio hilo kubwa akiliwakilisha taifa.

Amesema ni ngumu kwa baraza kumpatia mapokezi kwa kuwa hawana taarifa rasmi za ujio huo na hata alipoondoka hakuaga.

"Tunampongeza sana lakini taarifa za ushindi wake tumezipata kwenye vyombo vya habari, hata kurudi pia tunasikia mitandaoni hapo tunaandaa vipi mapokezi ya heshima,"amesema.

Mngereza amewataka wasanii wote nchini kuwa karibu na chombo hicho kwani kimeundwa maalum kwa ajili yao hivyo ni muhimu wanapokwenda nje ya nchi kwa ajili ya programu zozote za kuliwakilisha taifa wawe wanaaga na kutoa taarifa.



Chanzo; Mwananchi
 
Kutakuwepo na msafara utaopita mitaa mbalimbali?

Yote hayo ni kwa sababu ya kushinda hicho ki category ambacho hata hakionyeshwi kwenye award show?

Kweli watu walio deprived na success hata visivyo vya maana wataviona ni kama mana!
 
Huyu rayvanny ana umri wa miaka mingapi eti wadau!?
 
Kwani zile nyimbo wanazozifungia si wanazisikiaga kwenye vyombo vya habari hivyohivyo au?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…