Rayvany na Diamond wimbo wa Mwanza uko chini ya kiwango, BASATA kazi kwenu

Unajua sisi waafrica tumezoea kulalamika sana, sasa mleta mada anataka wimbo wa Diamond ufungiwe... Nikamwona kama ni mtumwa kwani ukiachana na diamond hamna mwanamziki mwingine, basi wote tusklize nyimbo za kaswida na nyimbo za dini
Msikilize diamond na hata Mimi namsikiliza ni mtanzania mwenzetu ila inapokosea lazima tuseme na akifanya vizuri tutamsifia pia
Wewe ni Aina was watanzania wanaopenda kusifia Kila kitu hata Kama hakipo sawa ili mradi tu unampenda,
Diamond ana nyimbo nzuri Sana nyingi tu Kama ukimuona , I miss you na nyingine kibao
 
Mkuu umewasikia BASATA? Maana watu Kama nyie kasi yenu ni kusifia ujinga tu kwasababu unampenda mtu

Hakuna tamko rasmi lolote lile la basata liliotoka

izo tetesi za kufungiwa hata wewe unaweza ukaandika humu na wau wakakuamini
 
Ulishawahi kuyaweka katika lugha ya KISWAHILI hayo maneno wanayoimba wakina Davido na Wizkid?
Si tu kufuatulia maana ya tungo za wakina davido na wizkid , Mimi ni mmoja wa watanzania tunaofuatilia mziki wa bara la Africa .



Kwa kukuelesha tu Davido au Wizkid kuimba matusi si Justification ya Diamond kuimba matusi. Kosa ni kosa tu. Yaani wewe Mke wako aende kupigwa mashine na jirani halafu ajitetee mbona Mama Jenifa nae alitembea na mtu flani na mume wake hakusema lolote. Kwa akili zako naona unaweza kutoa msamaha uliotukuka kwa huyo Mke wako aliotoka kupandia dhakari ya jirani yako.



Sasa turudi kwenye point, hao wakina Wizkid na Davido wameshafungiwa nyimbo zao nyingi tu huko Nigeria. Nakuwekea orodha hapa ujisomee na sio kuja na utetezi mbuzi.

 
Hivi unajua kusoma vizuri kweli Kiongozi?
Yaani umesoma vizuri,kisha ukaona kabisa bandiko langu linamtetea Diamond?
Acha kukurupuka,huyo niliyemjibu alikua anasema Diamond awaige akina Wizkid na Davido(akimaanisha hao jamaa wanafanya muziki unaofuata maadili mema),ndio nikamuuliza HAO AKINA WIZKID HAWAIMBI MATUSI?
Sijasema hiyo ni justification ya Diamond kuimba matusi.
Uwe unatulia kwanza kabla ya kumquote mtu.
 

Wasanii siku hizi sijui wanaimba nini,uchafu mtupu!
Ni ngono ngono tu.
Nani anakulazimisha kusikizwa ?
Stick kwa Rose Muhando na Christina Shusho au Bonny Mwaitege.
 
bwana wee waachie wenyewe nuimbo zao . hizi so nyimbo za kusikiliza😱😱😱😱😱😱😱
 
Nani anakulazimisha kusikizwa ?
Stick kwa Rose Muhando na Christina Shusho au Bonny Mwaitege.
Mkuu kuna pahala nimesema nalazimishwa?

Ama kama mimi sisikilizi ndio vitoto vidogo viharibiwe kwa kuimbishwa matusi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…