Nyambala
JF-Expert Member
- Oct 10, 2007
- 4,465
- 1,171
Tanzania zaidi ya uijuavyo, inaonyesha watanzania kampeni za namna hii ndiyo unawapata. Kwa kumbukumbu Raza si wa kwanza kuahidi kusacrifice mshahara wake!
Raza: Mshahara wa urais nitawapa wasiojiweza
na Tamali Vullu, Zanzibar
MGOMBEA urais Zanzibar, Mohamed Raza, amesema akifanikiwa kuwa rais wa Zanzibar mshahara wake wote ataupeleka kwa watu wasiojiweza ili waweze kuondokana na hali ngumu ya maisha. (Really???????)
Raza alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki mjini hapa alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu ya kuwania kurithi nafasi hiyo inayoshikiliwa na Rais Aman Abeid Karume.
Raza ambaye ni mfanyabiashara maarufu Zanzibar, alisema kitendo hicho kwake hakitakuwa cha kwanza kwani alipokuwa mshauri wa Rais Salmin Amour katika kipindi chote cha miaka sita hajapata kutumia mshahara wake bali aliuelekeza kusaidia wazee, watu wenye ulemavu na katika nyumba za ibada.
Nilipokuwa mshauri wa rais sikugusa mshahara wangu hata siku moja na hata mafao yangu sikuyagusa niliyapekeka kusaidia wazee, walemavu na nyumba za ibada na niliamua kufanya hivyo kutokana na kwamba Wazanzibari ndio walioniwezesha kufika hapa, alisema Raza.
Mambo mengine aliyopanga kuyafanya akiwa rais ni kuongeza maadili ya viongozi, kwani anaona yameporomoka kwa kiwango kikubwa na kuwatengenezea mazingira mazuri mawaziri na watendaji wengine wa serikali ili kukabiliana na tatizo la rushwa.
Ili kukabiliana na tatizo la rushwa miongoni mwa mawaziri na watendaji wengine wa serikali nitawatengenezea mazingira mazuri kwa kuwakopesha, ili kujenga nyumba kama hawana na kufanya vitu vingine vya kujiendeleza ili isiwe rahisi kwao kudanganyika kwa kupokea rushwa, alisema.
Kwa upande wa kukabiliana na matumizi mabaya ya fedha za umma, Raza atajitahidi kupunguza msafara wa magari ya rais.
Mfanyabiashara huyo amempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kuleta mafanikio makubwa nchini na kwamba atakuwa na muda mzuri wa kuyaendeleza mengine yaliyosalia katika kipindi kingine cha miaka mitano ijayo na alimsifu Rais Karume kwa jihitada mbalimbali za kuiendeleza Zanzibar.