RC amtimua mbunge kikaoni!

RC amtimua mbunge kikaoni!

n00b

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2008
Posts
1,015
Reaction score
2,680
* Ni kwa kuongea na simu wakati wa mkutano

Na Fadhili Abdallah, Kigoma

MKUU wa mkoa wa Kigoma, Joseph Simbakalia, amemtimua kwenye kikao cha Bodi ya Barabara mbunge,Sijapata Nkayamba (Viti Maalum – CCM) kwa kuongea na simu wakati kikao kikiendelea.

Kabla ya hatua hiyo, Simbakalia na wajumbe wengine wa kikao hicho, walilazimika kumvumilia mbunge huyo kutokana na simu zake kuathiri mwenendo wa kikao kwa kutoa milio yenye kelele kila mara.

Kama haitoshi, moja ya simu ya mbunge huyo iliita ambapo aliamua kuipokea na kuanza kuongea hali iliyoonekana kuingilia utulivu na usikivu wa wajumbe.

Hali hiyo ilimfanya, Simbakalia kumuagiza mbunge huyo kutoka kwenye kikao na kwenda kuongea na simu zake na kwamba angeruhusiwa kurudi baada ya kumaliza maongezi na simu hizo kuzizima.

Baada ya kuongea kwa muda, mbunge huyo alimweleza mkuu wa mkoa kwamba amemaliza na kuomba kikao kiendelee, lakini Simbakalia alishikilia msimamo wake wa kumtaka mbunge huyo kutoka ukumbini kwanza.

Kufuatia hali hiyo, kikao kilisimama kwa dakika kadhaa wakati wajumbe wakisubiri kutekelezwa kwa amri hiyo ya mkuu wa mkoa Kigoma ambaye alikuwa mwenyekiti.

Hatimaye mbunge huyo alilazimika kutoka nje ya ukumbi wa mikutano uliopo ofisi za mkuu huyo wa mkoa eneo la Mnarani mjini Kigoma.

Serikali imeshatoa maelekezo ambayo yamekuwa yakibandikwa kwenye kumbi mbalimbali za mikutano na wakati mwingine kutolewa kwa tangazo la kuwataka wajumbe wa vikao na hata watu binafsi kuzima simu zao au kutoa milio ili kuepuka usumbufu.
 
Angemcharaza bakora ili na wengine waone mfano.
 
Angemcharaza bakora ili na wengine waone mfano.
Mimi hii imenivunja mbavu sana. Nikawakumbuka wenzangu na mimi ambao hupokea simu hadi kanisani
 
Angemzaba vibao tu.
Wabeijing bwana yeye anaona ni haki kabisa kulonga na kimeo kwenye kikao.
Kwa vile ni mbunge wa kubebwa anajiona ndo mkubwa angekuwa naibu waziri je si angesimamisha kikao alonge na kimeo hicho kwanza.
 
Sijapata Nkayamba (Viti Maalum – CCM)

Mwenyewe huyu anamchango wowote kwa wananchi anapo kuwa Bungeni amewahi changia hoja kweli huyu hata kuuliza swali mi sijawahi msikia...huyu mzigo tu.
 
Huu ni ulimbukeni umetukumba wa-Tanzania,kila mtu kila mahali analonga longa tuu,Hebu fikiria ndani ya daladala kila abiria akiongea na simu kutakalika kweli.Nyumba za ibada je?Hatuna ustaarabu wa kujua tuongee wapi na simu na wakati gani.Twende pale kijiweni kwetu nako kila mmoja na kilonga longa chake,tutawasikiliza waheshimiwa kweli kwa jinsi hiyo?TUWENI WASTAARABU TU.
 
Angemzaba vibao tu.
Wabeijing bwana yeye anaona ni haki kabisa kulonga na kimeo kwenye kikao.
Utakuta simu yenyewe ya kichina na inaita kwa mwimbo wa taarab.

Job true true!
 
Angemzaba vibao tu.
Wabeijing bwana yeye anaona ni haki kabisa kulonga na kimeo kwenye kikao.
Kwa vile ni mbunge wa kubebwa anajiona ndo mkubwa angekuwa naibu waziri je si angesimamisha kikao alonge na kimeo hicho kwanza.

Angemcharaza bakora ili na wengine waone mfano.

Najiuliza, angalikuwa huyo mbunge ni mwanaume kutoka jimboni. Kweli mngetoa maoni haya?
 
Najiuliza, angalikuwa huyo mbunge ni mwanaume kutoka jimboni. Kweli mngetoa maoni haya?

Hushangai wanaotuhumiwa kusababisha ajali ya treni wako rumande ila Chenge aliyeuwa wanawake wawili yuko numbani! Case by case baba 😕
 
Huyu mama anahitaji kuhurumiwa, nahisi anamatatizo fulani kichwani, hata baadhi ya michango yake bungeni huwa hai make sense kabisa. Nahisi ana frustration flani, walio karibu naye wanaweza kutusaidia, kwa upande wangu naungana na Fidel80 kuwa huyu....ni mzigo, siyo kwa sababu ni mwanamke ila kwa sababu ya tabia zake.
 
Tena bado kaonewa huruma kuambiwa akaongee akimaliza azime simu arudi kikaoni. Angeambiwa atoke na asirudi kikaoni tena mpaka aombe radhi.
 
Huyu mama anahitaji kuhurumiwa, nahisi anamatatizo fulani kichwani, hata baadhi ya michango yake bungeni huwa hai make sense kabisa. Nahisi ana frustration flani, walio karibu naye wanaweza kutusaidia, kwa upande wangu naungana na Fidel80 kuwa huyu....ni mzigo, siyo kwa sababu ni mwanamke ila kwa sababu ya tabia zake.

Basi hakustahili kuteuliwa kama mbunge. Sijui Rais alitumia vigezo vipi kuwateua Wabunge hawa.
 
Back
Top Bottom