RC awaka nyaraka za AMCOS kutuzwa kwenye Jaba

RC awaka nyaraka za AMCOS kutuzwa kwenye Jaba

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewataka Viongozi wa Chama cha Msingi Kisuke katika Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama kusitisha utunzaji wa nyaraka za ofisi katika Jaba lililokuwa katika Ghala la kuhifadhia Zao la Pamba.

RC Macha ametoa agizo hilo leo wakati akiendelea na ziara ya kutembelea Wakulima na kukagua maendeleo ya zao pamba katika Halmashauri hiyo na kubaini uwepo wa uzembe katika utunzaji wa nyaraka za Amcos hiyo yenye jumla ya Wakulima 100.

Soma: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Emmanuel Cherehani amewashauri viongozi wa AMCOS kuwa na desturi ya kutatua changamoto katika maeneo yao bila kusubiri viongozi wa ngazi za juu ikiwa ni pamoja na kutunza vyema nyaraka na pembejeo.

 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anamringi Macha, ameeleza kushangazwa na uhifadhi holela wa nyaraka za wakulima wa zao la pamba katika Chama cha Msingi (AMCOS) cha kijiji na kata ya Kisuke, Halmashauri ya Ushetu, ambapo nyaraka hizo zimehifadhiwa ndani ya jaba la maji bila kuwa na taarifa rasmi za mapato, matumizi, na uzalishaji wa zao hilo.

Tukio hilo limeibuka jana wakati Macha alipomtaka Mwenyekiti wa chama hicho, Cosmas Shija, awasilishe taarifa ya uzalishaji wa pamba, idadi ya wakulima, pamoja na pembejeo na viuatilifu vilivyopokelewa. Hata hivyo, alibaini kuwa nyaraka hizo zimehifadhiwa kiholela ndani ya ghala la pamba.

Shija alieleza kuwa wamehifadhi nyaraka hizo kwenye jaba la maji kwa sababu ya ukosefu wa mahali salama pa kuzihifadhi. Aidha, alisema chama hicho hakina taarifa ya mapato na matumizi kutokana na mapato yao kushuka tangu Agosti mwaka jana.

"Ni kweli nyaraka tunazihifadhi kwenye jaba la maji lililopo ndani ya ghala la pamba. Hatuna taarifa za mapato na matumizi kwa sababu mapato yetu yameshuka tangu Agosti mwaka jana, ambapo tulipata Shilingi 200,000 pekee na tukashindwa kujenga ofisi ya kuhifadhi nyaraka," alisema Shija.
Screenshot 2025-01-31 105424.png


Kwa upande wake, Katibu wa chama hicho, Letisia Daudi, alisema kuwa walipokea tani 6.5 za mbegu na kuzigawa kwa wakulima 135 kwa uwiano sawa, ambapo kila mkulima amelima hekari moja ya pamba. Aliongeza kuwa hivi karibuni wamepokea bomba 30 za kupulizia dawa kwa ajili ya kudhibiti wadudu waharibifu wa mazao.

Mkuu wa Mkoa, Macha, aliwataka viongozi hao kuandaa taarifa kamili kuhusu uzalishaji wa pamba, pembejeo na viuatilifu vilivyopokelewa, pamoja na taarifa za mapato na matumizi. Alisisitiza kuwa taarifa hizo zinapaswa kuandaliwa kwa kushirikiana na afisa kilimo wa kata na kuziwasilisha kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhitaji, badala ya kutumia kigezo cha kushuka kwa mapato kama kisingizio cha kutokuwa na rekodi sahihi.

Aidha, aliahidi kuwapatia viti na meza maalum kwa ajili ya kuhifadhi nyaraka za wakulima, akiwataka waache kuzihifadhi kiholela ndani ya jaba la maji. Pia aliwataka viongozi wa Amcos kufanya vikao vya mara kwa mara ili kuwasikiliza wakulima na kuwasilisha changamoto zao kwa Bodi ya Pamba kwa ajili ya kutafutiwa suluhisho.

Chanzo: Nipashe
 
Back
Top Bottom