Ndagullachrles
Senior Member
- Jun 20, 2023
- 153
- 161
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Nurdin Babu amezindua msimu wa tano wa Tamasha la Kahawa(Kahawa Festival) na kutoa wito kwa wananchi kujikita kwenye uzalishaji wa zao la Kahawa.
Amesema zao la Kahawa lilichangia kwa kiwango kikubwa kufanikisha maendeleo ya mkoa ikiwamo kuwa na shule nyingi za sekondari ambazo zilitoa wasomi wengi.
Amesema kuwa kwa sasa kilimo cha zao la Kahawa katika mkoa wa Kilimanjaro kimeshuka kutokana na sababu mbali mbali ikiwamo mabadiliko ya tabianchi,ufinyu wa ardhi na kupanda kwa gharaza za uzalishaji ikiwamo pembejeo za kilimo.
"Miaka ya nyuma Kilimanjaro ilikuwa inaongoza kwa kilimo cha Kahawa,Kahawa imesomesha watoto wengi wa wakulima na tunao wataalamu wengi wakiwamo maprofesa,hawa wote wametokana na kilimo cha Kahawa".amesema.
"Kahawa imejenga shule nyingi sana na sasa naomba wale mnaoishi ukanda wa juu mhamie ukanda wa chini ambako kuna ardhi ya kutosha,huko mtapata maeneo ya kujenga na ukanda wa juu mkatumie kwa killimo cha Kahawa",amesema..
Babu ametoa wito wa wananchi wa Kilimanjaro kuzalisha Kahawa yenye ubora Ili kukabiliana na soko la Kahawa duniani.
Katika kufikia lengo la aslimia 15 ya unywaji wa Kahawa mkuu wa mkoa alisema lazima juhudi ziongezwe ikiwamo ushirikishwaji wa wakulima.
Mapema mwenyekiti wa kamati ya Kahawa Festival ,Denis Mahulu alisema Tamasha hilo linalenga kuongeza unywaji wa Kahawa kwa soko la ndani na kufikia aslimia 15.
Tamasha hilo linatarajia kufanyika mwezi ujao kwenye kiwanda cha kukoboa Kahawa cha Tanganyika Coffee Curing kuanzia oktoba 4 hadi oktoba 6.