RC Byakanwa aongoza mazoezi na wana Tandahimba

wandamba

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Posts
510
Reaction score
839
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Gelasius Byakanwa Leo Jumamosi Machi 16, 2019 aongoza mazoezi ya viungo na wakazi wa wilaya Tandahimba.

RC Byakanwa akiongozana na mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya Tandahimba Mhe. Sebastian Waryuba walianza mazoezi pamoja na Viongozi na Wananchi kwa kukimbia na kisha kumalizia na mazoezi ya viungo yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya msingi ya Amani iliyopo kata ya Tandahimba Wilaya ya Tandahimba.

Akizungumza mara baada ya kumaliza mazoezi RC Byakanwa alisisitiza umuhimu wa kufanya mazoezi ili kuimarisha afya ya akili na mwili na hivyo kujiepusha na magonjwa ya moyo na kisukari.

*"Mazoezi ni muhimu sana kwa afya zetu kwani yanatuepusha na magonjwa ya moyo na kisukari na pia huimarisha afya ya akili."* Alisema RC Byakanwa.

RC Byakanwa yupo kwenye ziara ya siku moja kwa ajili ya kuhamasisha zoezi la vitambulisho vya Wajasiliamali wadogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…