RC Chalamila aagiza Majina ya Wafanyabiashara 891 yaondolewe kwenye mtandao wa Shirika la Masoko Kariakoo kupisha Uchunguzi

Black Butterfly

Senior Member
Joined
Aug 31, 2022
Posts
130
Reaction score
368
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Albert Chalamila ameagiza kuondolewa majina 891 ya wafanyabiashara yaliyowekwa kwenye mtandao wa Shirika la Masoko Kariakoo mpaka pale vyombo vya dola vitakapojiridhisha na majina hayo.

Hatua hiyo inakuja baada ya wafanyabiashara zaidi ya 800 waliokuwepo sokoni hapo kabla ya soko kuungua Julai 2021 kuandamana jana Alhamisi, Julai 11, 2024 kwenda Ofisi za CCM Lumumba kupinga kutorejeshwa.

Katika orodha hiyo, wafanyabiashara 891 kati ya 1,861 ndio walioelezwa kuwa na vigezo vya kurejea. Uamuzi huo uliwafanya kujitokeza katika viwanja vya Mnazi Moja kuhakikiwa na baada ya kutoridhishwa ndio wakaandamana.

Chalamila ametoa maagizo hayo leo Ijumaa Julai 12, 2024, alipozungima na uongozi wa Shirika la Masoko Kariakoo katika Ofisi ya Shirika la Masoko Magogoni.

Mbali na hilo, Chalamila ameagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza malalamiko ya wafanyabiashara kuwa majina hayo yamewekwa kwa njia za rushwa huku akiwataka viongozi wa Shirika la Masoko kujitafakari.

MWANANCHI
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amefuta zoezi la awali la uhakiki wa majina ya wafanyabiashara 892 waliahakikiwa na shirika la masoko ya kariakoo na kutaka zoezi hilo lianze upya kwa njia ya Kidijiitali, ili kuondoa manunung'uniko na malalamiko ya Wafanyabiashara wanaopaswa kuingia ndani ya soko hilo ambalo ujenzi wake uko mbioni kukamilika.
ITV.jpg

============

Back
Top Bottom