The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila kwa niaba ya serikali ya mkoa huo ameanzisha hamasa ya kuanzisha mfuko mahsusi kwa ajili ya wasanii wa 'maigizo' pekee ambapo kwa kuanzia itatolewa milioni 15 kwa ajili ya mfuko huo
Chalamila ameeleza hayo leo, Jumatatu Novemba 04.2024 alipotoa salamu za rambirambi za msiba wa aliyekuwa msanii maigizo wa muda mrefu nchini Grace Mapunda (Tesa) kwenye viwanja vya Leaders club, jijini Dar es Salaam ambapo mfuko huo ni tofauti na ule unaoendeshwa na serikali unaohusisha wasanii wote
Pia, soma: Muigizaji Grace Mapunda (Tessa) amefariki dunia
"Nilikuwa namuuliza Mwenyekiti wa Waigizaji wote; mimi ni mfuasi mkubwa wa Sanaa za maigizo na nilipokuwa mdogo niliigiza sana. Nikamuuliza, je, wasanii mna mfuko? Akasema tuna mfuko. Mfuko huu ni ule ambao Mh. Rais ameweka fedha nyingi ili ninyi wasanii wa sekta mbalimbali muweze kutumia kupata mikopo..
....Lakini nikauliza tena, je tasnia ya Sanaa ya maigizo in mfuko? Akasema haina mfuko. Kwahiyo Mwenyekiti, sisi Mkoa wa Dar es Salaam tutawakabidhi milioni 15 tufungue mfuko kumuenzi dada yetu Grace Mapunda.
Na mfuko huu ambao wewe pamoja na wenzako mtauanzisha, lakini kabla hamjauanzisha tutadute siku tukae na hao waigizaji wote. Isipite zaidi ya wiki mbili, tukae na niwakabidhi pesa yenu. Na Mh. Naibu Waziri ambaye yupo hapa, Ndugu yangu Mwana FA, yeye atawasaidia na kuwa-guide ili mfuko huo uo-perate.."