RC Chalamila amezindua mpango wa upanuzi na uboreshaji wa Hospitali ya Amana wa Bilioni 3. Huduma ua Kangaroo kuwa bora zaidi

RC Chalamila amezindua mpango wa upanuzi na uboreshaji wa Hospitali ya Amana wa Bilioni 3. Huduma ua Kangaroo kuwa bora zaidi

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amezindua mpango wa upanuzi na uboreshaji wa Hospitali ya Rufaa ya Wilaya ya Ilala ya Amana (yenye hadhi ya Mkoa) utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni tatu.

Ni katika muktadha huo Chalamila amewataka wadau wa maendeleo na wananchi kushirikiana na Serikali kutimiza lengo hilo ili kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa mpango wa upanuzi na uboreshaji wa majengo ya hospitali hiyo ya yufaa, Chalamila amesema Serikali ya Awamu ya Sita ina nia ya kuimarisha huduma za afya hivyo amewataka wadau wa maendeleo na wananchi kwa ujumla kushiriki mpango huo ambao harambee yake itafanyika Agosti 31 katika ukumbi wa Mlimani City jijini humo.

Chalamila ameongeza kuwa moja ya njia za kutoa sadaka kwa Mungu ama kurejesha kwa jamii faida ni pamoja na mpango huo wa upanuzi na uboreshaji wa huduma za afya kama huo wa kuboresha hospitali ya Amana kwa ajili ya ustawi wa wananchi.

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Amana iliyopo Dar es Salaam Dkt. Bryceson Kiwelu amesema kupitia miradi ya kimkakati ya zaidi ya shilingi Bilioni tatu ikiwemo wodi itakayokuwa na vifaa vya kisasa, itasadia kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Dkt.Kiwelu amebainisha hayo wakati wa uzinduzi wa harambee maalumu iliyoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila kwa lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kuboresha huduma ya mama na mtoto katika hospitali hiyo."Kama taasisi tumeona ipo haja kuwa na miundombinu bora na ya kisasa kuwezesha uzazi salama ambapo mama mjamzito atakaa na shangazi kwenye chumba cha kujifungulia chenye faragha na mkakati wa muda mrefu ni kujenga jengo lenye uwezo wa kubeba vitanda 350 pamoja na vyumba vya upasuaji na kuhakikisha kwamba Watanzania wanapata huduma iliyo bora". Amesema Dkt.Kiwelu

Amesema moja ya mambo yaliyofanyika kwa ajili kuboresha huduma ya mama na mtoto ni kufanya tafiti za ndani kuangalia jinsi ambavyo hospitali inaweza kutoa huduma kwa viwango vya kimataifa."Takwimu za ndani zinaonesha kuwa tukiwekeza kwenye huduma ya Kangaroo Mother Care, yani pale ambapo mama anamkumbatia mtoto, tuna nafasi kubwa sana ya kupunguza vifo kwa sababu mama ni kama daktari wa kwanza, maana akiona mtoto amebadilika ni rahisi kumjulisha muuguzi au daktari na hatua kuchukuliwa".Amesema Dkt. Kiwelu

Ameongeza kuwa huduma ya Kangaroo ni bora mara tatu zaidi ya huduma ya mtoto kulala peke yake, hivyo hospitali ya Rufaa ya Amana imekuwa ikijitahidi kuhakikisha kwamba vitanda vya kangaroo vinamwezesha mama kulala na mtoto wake na hivyo kupunguza hatari ya mtoto kufariki dunia.
 
Back
Top Bottom