RC Chalamila aonya wanaotumia janga la Kariakoo kutapeli watu, "Sio muda wa kujinufaisha, Kuchuliwa hatua kali"

RC Chalamila aonya wanaotumia janga la Kariakoo kutapeli watu, "Sio muda wa kujinufaisha, Kuchuliwa hatua kali"

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amewaonya baadhi ya Watu wanaotumia janga la kuporomoka kwa ghorofa Kariakoo kutapeli kwa kuchanganisha michango kinyume na taratibu kuacha mara moja akisema wanaweza kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Pia, Soma: Maafa Kariakoo: Usichangishe fedha tumia akaunti ya Serikali

RC Chalamila amesema "Nitoe rai kwamba tumekwishaanza kupata minong’ono ya baadhi ya Watu kuanza kutumia tukio hili kinyume na utaratibu na sheria zilizopo za maafa kwa wote ambao wanatumia mwanya kutapeli Watu kuwa na ‘lipa namba’ ambazo hazijthibitishwa ama kuwa na ‘lipa namba’ ambazo wanatumia jina la Serikali kujinufaisha naomba nitoe rai kwamba wanaweza kuchukuliwa hatua kali za kisheria"

"Muda huu sio wa kujinufaisha bali ni wa kuwaokoa wenzetu, sisi kama Serikali na Mhe. Rais amekwisha elekeza kwamba gharama zote za msingi zibebwe na Serikali na Ofisi ya Mhe. Waziri Mkuu ndio itakayoratibu masuala yote ya gharama kuanzia majeneza hadi usafiri"
 
mil1-tzmsaadatouturuki.jpg


to jamii forums.jpg

2023


IMG-20241118-WA0010.jpg

2024
 
Back
Top Bottom