johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Mkuu wa mkoa wa DSM Albert Chalamila amewataka wananchi wa DSM kujilinda wao na familia zao dhidi ya matukio yoyote yanayoweza kuhatarisha Amani na Usalama wao
RC Chalamila amesema SI HAKI kuwatupia lawama Polisi kwa kila Jambo.
---
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amewataka Wakazi wa Dar es salaam kutambua umuhimu wa kujilinda na kuzilinda Familia zao dhidi ya matukio yoyote yanayoweza kuhatarisha amani na usalama wao badala ya kuwatupia lawama Polisi kwa kila jambo.
RC Chalamila amesema hayo wakati akifanya ziara ya kukagua Zahanati ya Kurasini Wilayani Temeke leo September 27,2024 “Leo kwenye mkutano nitaongea baadhi ya vitu ambavyo Watu wanalalamikia utekaji sijui nini, leo kwenye mkutano nitawapa data namna Vijana wetu tuliowazaa wanavyoshiriki kwenye baadhi ya matukio, nitawapa tukio la Mama ameuawa na kuchinjwa vipande karibu 30, wa hapahapa Temeke Mbagala na aliyefanya na nitawaeleza alifanyaje”
“Nitawapa matukio ya Watu wameenda kwa Waganga wa kienyeji, Mganga ameona wana hela akawanywesha sumu wakafa akaiba hela akawazika bila taarifa, leo mnapokuta kuna matukio Watu wanasema Polisi ndio wanateka, Vyombo vya Dola vinateka, kuna vitu mnakosa uelewa na kwasababu mnakuja kwa mihemko hamuwezi kujibiwa kistaarabu hata kidogo”
"Halafu kwa mashinikizo mnasema tunataka kuingia barabarani, lazima Serikali iseme, kama tunataka kujenga Taifa letu ni vizuri tujenge mijadala ya kuulizana maswali, kuna vitu vinafanyika kama sanaa kuna vingine kweli Watu wamefanya, ebu niwaulize Baba na Mama wamefunga mlango wamekwenda ndani kulala asubuhi unaambiwa uko ndani Watu wameuana hivi niambieni kwenye mazingira hayo Polisi wanahusikaje?
kwahiyo Polisi awaambie laleni Mimi nipo mlangoni mpaka kunakucha inawezekana jamani?, kwahiyo Mlinzi wa kwanza kwa kila jambo ni Mwananchi mwenyewe”
“Hata Mimi Mkuu wa Mkoa unaweza kukuta hapa nalindwa lakini hawa wanaonilinda nakuwa nao nyumbani?, kama Mimi nitaondoka kwangu na Mkuu wa Wilaya tunakwenda huko Mbagala kunywa pombe tukishakunywa pombe tunachukua Wake za Watu halafu nasema watatufanya nini, watatupiga makofi huko na watanichinja, kwahiyo ulinzi wa kwanza ni wewe mwenyewe Raia”
“Mtu unazaa Mtoto huelewi ameenda wapi kutoka asubuhi hadi jioni, inafika saa mbili ndio unasema mtafuteni Mtoto, hivi kweli Mtoto huyo alikaa kwenye tumbo lako au la jirani?”
Pia soma
- RC Chalamila: Matukio ya Mauaji na Utekaji Watoto yapo lakini siyo kama yanavyoripitiwa, mengi siyo ya kweli
Source: Ayo TV