RC Chalamila: Baadhi ya Matendo Polisi hawahusiki. Ulinzi wako sharti ujilinde mwenyewe

RC Chalamila: Baadhi ya Matendo Polisi hawahusiki. Ulinzi wako sharti ujilinde mwenyewe

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Mheshimiwa waziri mkuu kuna tukio limetokea hapa mwezi uliopita kuna bwana mmoja alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mama mmoja katika kugombana kwao yule bwana kamdanganya yule mama kamchukua akaenda kumchinja na baada ya kuona haitoshi akamcharanga vipande na akaenda kutupa viungo sehemu tofauti tofauti baada ya siku tatu wananchi wakaanza kupiga kelele Askari wamemteka mama.

Baada ya kufuatilia jeshi la polisi na vyombo vingine vya dola kuchunguza vimesha mbaini yule bwana aliefanya hivyo na amekiri kufanya. Kwa hivyo baadhi ya matendo yanayofanyika wakati fulani hata hayalihusu kabisa jeshi la polisi. Baba na mama wamegombana ndani wakitoka nje wanasema jesho la polisi haliwajibiki” Albert Chalamila

“Hata mimi mkuu wa mkoa pamoja na nimepewa walinzi nikatoka nikaja kunywa pombe huku Temeke nimesha lewa naanza kusema mtanifanya nini halafu natoka naiba wake wa watu, nitakatwa makofi ikiwezekana naweza nikachinjwa hapa hapa hadharani. ulinzi wa mwanadamu sharti ujilinde wewe mwenyewe.

Boda boda endesha pikipiki kwa ustaarabu mama lea mwanao vizuri, kwa hiyo ni kweli kulikuwa na hivyo vitendo vidogo vidogo lakini kwa silimia kubwa tunavidhibiti” Amesema Mkuu wa mkoa Dar es Salaam Albert chalamila

PIA SOMA

- RC Chalamila awataka wakazi wa DSM wajilinde Wao na familia zao dhidi ya matukio hatarishi badala ya kuwatupia Polisi lawama
 
Back
Top Bottom