Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila akizungumza na wanahabari leo, Jumatatu Novemba 25.2024 ametoa wito kwa wakazi wa jiji hilo waliojiandikisha kwenye daftari la mkazi kujitokeza kwa wingi kupiga kura Novemba 27.2024 ili kuchagua viongozi wa serikali za mitaa wanaowataka.
Sambamba na hilo Chalamila ametoa rai kwa wakazi wa Dar es Salaam na wadau wa uchaguzi kwa ujumla wake kujiepusha na siasa za chuki.