RC Chalamila: Msemaji Mkuu wa Serikali kutoa taarifa kuhusu mwenendo wa Uokoaji maafa ya Kariakoo na siku ya kufungua maduka

RC Chalamila: Msemaji Mkuu wa Serikali kutoa taarifa kuhusu mwenendo wa Uokoaji maafa ya Kariakoo na siku ya kufungua maduka

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaamm, Albert Chalamila, amesema kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali atatoa taarifa rasmi kuhusu mwenendo wa zoezi la uokoaji katika eneo la Kariakoo, ambapo maafa yalitokea hivi karibuni.

Chalamila ameeleza kuwa zoezi la uokoaji linaendelea na taarifa kamili kuhusu hali ya jumla ya uokoaji pamoja na tarehe kamili ya kufunguliwa kwa maduka ya karibu na eneo lililoathiriwa, zitatolewa katika siku mbili zijazo. Amesema kuwa maelezo hayo yatatolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu na yatafafanua hatua zote zilizochukuliwa katika mchakato wa kurejesha hali ya kawaida.
 
Back
Top Bottom