LGE2024 RC Chalamila: Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Utafanyika katika Mitaa yote 564 ya Dar kwa Uhuru na Haki

LGE2024 RC Chalamila: Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Utafanyika katika Mitaa yote 564 ya Dar kwa Uhuru na Haki

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
"Rais Samia Suluhu Hassan ni mwana demokrasia wa kwanza katika Nchi yetu, kwahiyo ni wito wake kuwaomba watanzania na wana Dar es Salaam wote kuhakikisha Tunashiriki kwa kiasi cha kutosha ili tuweze kichagua Viongozi tunaowataka, na mwisho tuepuke malalamiko kwa kuchagua au kwa kutohusika kuchagua viongozi ambao hawatakuja kuwa na msaada kwetu. Kuwa chama cha upinzani au kuwa chama chochote cha kisiasa si Ugomvi katika Nchi ya Tanzania bali ni utamaduni wa kikatiba unaotaka Mgombea wa aina yoyote, kwanza awe na Itikadi ya Chama kitakachompitisha kuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti au wajumbe watano"

Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Uchgauzi wa Serikali za Mitaa Utafanyika katika Mitaa yote 564 ya Mkoa wa Dar kwa Uhuru na Haki. Ameyasema hayo leo tarehe 06 Julai 2024 Wakati akiongea na Wanahabari Ofisini kwake Dar.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024, wanaochaguliwa ni Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa pamoja na Wajumbe Watano [5] wanaounda Kamati ya Mtaa ambapo wapiga kura ni Wakazi walioko katika mitaa husika.

"Wakazi hao watatakiwa kujiandikisha katika vituo vilivyopo katika maeneo yao ya Makazi ili kujumuishwa katika ordha ya wapiga kura wataopiga kura siku ya uchaguzi huo". Amesema Chalamila

Mkuu wa Mkoa Chalamila amezitaja Sifa Muhimu za Mwananchi kujiandikisha na kushiriki uchaguzi huu ni pamoja na;-

Awe Raia wa Tanzania, Awe na Umri wa miaka 18 au Zaidi, Awe ni mkazi wa eneo la Kitongoji au Mtaa husika, Asiwe na ugonjwa wa akili uliothibitishwa na Daktari anayetambulika na Serikali au Bodi ya Utabibu na Awe amejiandikisha kupiga kura katika Kitongoji au Mtaa husika.

Chalamila amesema, OR-TAMISEMI imeshafanya uhakiki wa maeneo ya kiutawala na Mkoa wa Dar es Salaam umebakia na maeneo yake ya awali yanayojumuisha Wilaya 5, Tarafa 12, Kata 102 na Mitaa 564.

Hivyo uchgauzi huu wa Serikali za Mitaa Utafanyika katika Mitaa yote 564. Mgawanyo wa mitaa hiyo nika ufuatavyo;-

Wilaya ya Ilala Mitaa 159, Kinondoni Mitaa 106, Temeke Mitaa 142, Kigamboni Mitaa 67, Ubungo Mitaa 90.

"Tayari OR-TAMISEMI imeshatoa Rasimu ya Kanuni za Uchaguzi wa Seriali za Mitaa wa Mwaka 2024 na imeshakupokea maoni ya Wadau mbalimbali juu ya kanuni hizo na hivyo Kanuni halisi zinatarajiwa kutolewa hivi karibuni". Amesema Chalamila.

Tangazo la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024 litatolewa kwa kuzingatia Kanuni husika za Uchaguzi huo na litaonyesha taratibu za kuzingatiwa na ratiba yote ya utekelezaji wa zoezi la Uchaguzi pia aidha, hatua zinazoendelea ni pamoja na Maandalizi ya Vifaa mbalimbali vya uchaguzi, Uhakiki wa Vituo vya kuandikishia wapiga kura, ueleimishaji umma juu ya uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa

Mkoa pamoja na Halmashauri zote unaendelea kufanya maandalizi yote muhimu kwa ajili ya kuhakikisha uchanguzi huo unafanyika kwa ukamilifu na kila wananchi katika eneo husika anapata fursa ya kushiriki.

Chalamila amesema, Wananchi wanahamasishwa kushiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024 ambapo wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kuwa wapiga kura katika tarehe na vituo vitakavyoelekezwa pia kuhakiki majina na taarifa zao katika vituo vya kupigia kura katika tarehe na siku zitakazokuwa zimeelekezwa. Aidhaa, wananchi wanahimizwa kuendelea kufuatilia kwa karibu matangazo na maelekezo yatakayokuwa yanatolewa na OR-TAMISEMI, Viongozi wa Mkoa, Wilaya na Halmashauri kuhusu Uchaguzi huo.
 
Ni maneno tu hata kichaa yeyote anaweza kutamka. Tatizo ni sheria na Time ya usimamizi
 
Siku ya uchaguzi utasikia majina ya wapiga kura yamechelewa kufika
 
Back
Top Bottom