Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Bi. Happiness Seneda, pamoja na Viongozi mbalimbali wa ngazi ya Mkoa na Wilaya, wakiongozana na Wananchi wa Mkoa wa Songwe, wamewasili Mkoani Arusha, tarehe 19 Januari 2025 kwa ajili ya kushiriki mazishi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Ester Mahawe.
Ester Mahawe alifariki Dunia tarehe 14 Januari 2025 katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC), mkoani Kilimanjaro, alipokuwa akipatiwa matibabu. Mazishi yake yanatarajiwa kufanyika tarehe 20 Januari 2025.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
Pia soma ~ Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe, Esther Mahawe afariki Dunia