The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, leo Machi 4, 2025 amewaongoza wanawake wa Wilaya ya Singida kushiriki ujenzi wa shule ya amali ya mkoa huo inayojengwa kata ya Unyambwa Manispaa ya Singida kwa gharama ya Sh.bilioni 1.6 ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Akizungumza na wanawake waliojitokeza kushiriki ujenzi huo amesema halmashauri zote za mkoa huo zimepewa fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule ya amali lakini katika shule ya amali ya mkoa watachaguliwa kujiunga wanafunzi wenye vipaji.
Pia soma: Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze
Awali Mhandisi wa Manispaa ya Singida, Karisto Mligo, amesema ujenzi wa shule ya amali ya Mkoa wa Singida ambayo itakapokamilika katika awamu ya kwanza itachukua wanafunzi takribani 400 wenye vipaji watakaofundishwa ufundi wa aina mbalimbali na ujenzi wake unatarajia kukamilika Mei 29, 2025.