RC Dodoma aitaka TRC kuongeza mashine za ukaguzi wa risiti

RC Dodoma aitaka TRC kuongeza mashine za ukaguzi wa risiti

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameututaka uongozi wa TRC Dodoma kuongeza mashine za ukaguzi wa risiti za malipo kwa abiria na kutatua kero ya msongamano wa abiria pindi wanapotoka stesheni.

Senyamule ameyasema hayo alipotembelea stesheni kuu ya Usafiri wa Reli ya Kisasa (SGR) na kushuhudia malalamiko ya abiria ya upotezaji wa muda kutokana na uhaba wa mashine za kukagua risiti za malipo pindi wanapotoka katika stesheni hiyo

Soma Pia: Mchengerwa: Utaratibu unaotumika stesheni ya SGR Dodoma ni mbovu

Kupitia ziara hiyo ya mkuu wa mkoa wa Dodoma katika steshen ya Samia imeonekana Muingiliano wa watu , magari pamoja na wafanyabiashara wakati abiria wanaposhuka katika stesheni hiyo imekuwa mmoja ya sababu ya msongamano unaopelekea foleni na kukwamisha abiria kutoka kwa wakati.

 
Back
Top Bottom