Tripo9
JF-Expert Member
- Sep 9, 2009
- 4,357
- 3,550
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amesema kuna chanjo 15,000 za Uviko-19 hazijatumika mkoani humo huku kukiwa na changamoto kwa kuwa baada ya mwezi mmoja kuanzia leo Jumamosi Septemba 25, 2021 zitafikia mwisho wa matumizi yake.
Ameeleza kuwa mkoa umepata dozi 15,000 za chanjo ya Uviko-19 ambazo bado hazijatumika kati ya 30,000 zilizopokelewa, zitumike katika kipindi kifupi kijacho.
Kunenge amesema kwa kuanza wameamua kukutana na kamati ya afya ya msingi ngazi ya mkoa na wilaya, wataalamu kutoka Wizara ya Afya na Tamisemi ili kwa pamoja kufanya tathimini na kujipanga upya kwa kuongeza wigo mpana wa utoaji chanjo hiyo ili iishe yote kabla ya muda wake wa kuharibika haujafika.
"Chanjo hizi zina muda wake maalumu na tumeangalia mpaka sasa katika mkoa wetu katika chanjo 30,000 tulizopokea sasa hivi tumefikia asilimia 50 ya dozi hizi kwa maana zimetumia kama 15,000 tu , nusu ya chanjo hizo bado hazijatumika na ni mwezi mmoja tu umebaki lazima tutumie mbinu shiriki na hizi zitumike kwa hiyo kikao hiki ni kikao cha kutafuta majibu," amesema Kunenge akibainisha kuwa idadi ya waliochanja ni ndogo ikilinganishwa na wakazi wa mkoa huo huku akitaka wakuu wa wilaya kusimamia utoaji wa chanjo.
Chanzo: Mwananchi