Rc Kunenge tuambie ukweli juu ya vifo na idadi kamili iliyotokana na mkanyagano uwanja wa uhuru

Rc Kunenge tuambie ukweli juu ya vifo na idadi kamili iliyotokana na mkanyagano uwanja wa uhuru

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Inashangaza watu unakomaa kukanusha habari za wamachinga kulazimishwa kufunga maduka ili washiriki maombolezo ya kitaifa huku unaacha kukanusha kama kweli au si kweli watu 45 wamefariki na wengine mamia kujeruhiwa.

Huu sio wakati wa kuacha kuwapa Watanzania ukweli juu ya nini kinaendelea hapa nchini please nenda na matukio na wakati.
 
Inashangaza watu unakomaa kukanusha habari za wamachinga kulazimishwa kufunga maduka ili washiriki maombolezo ya kitaifa huku unaacha kukanusha kama kweli au si kweli watu 45 wamefariki na wengine mamia kujerujiwa.

Huu sio wakati wa kuacha kuwapa watanzania ukweli juu ya nini kinaendelea hapa nchini please nenda na matukio na wakati.View attachment 1731840
Hao wahuni wametumwa na nani sasa?
 
Huku Dodoma leo wenye maduka walipigwa Mkwara Mzito wa Maduka kufungwa.

One way yote Maduka yalifungwa, Soko la Majengo na Maeneo kuzunguka Uwanja wa Jamhuri Maduka yalifungwa kwa lazima.
 
Huku Dodoma leo wenye maduka walipigwa Mkwara Mzito wa Maduka.

One way yote Maduka yalifungwa, Soko la Majengo na Maeneo kuzunguka Uwanja wa Jamhuri Maduka yalifungwa kwa lazima.
Nasikia barabara zote zilikuwa zimefungwa kuingia na kutoka tangu asubuhi sijui wasafiri wamepataje shida leo.
 
Mh kama ni kweli huu mfumo tunaoenda nao hauna afya nzuri kwa maendeleo ya wananchi
 
Tatizo la viongozi wa Tanzania wanataka kila tatizo waletewe ofisini kwamba kuna hili limetokea au linatusumbua hawataki kufuatilia ukute hapo anasema hivo na hajafuatilia hata kidogo lazima upotoshe umma tu.
 
Mungu awarehemu tu wafiwa kwakweli, binafsi sioni haja ya kutangaza chochote kwasasa maana wananchi wenyewe ndio walikua wakaidi wa maagizo ya jeshi la polisi.
 
Mungu awarehemu tu wafiwa kwakweli, binafsi sioni haja ya kutangaza chochote kwasasa maana wananchi wenyewe ndio walikua wakaidi wa maagizo ya jeshi la polisi.
Kwa hiyo tuendelee kuamini wanaosema watu 45 wamefariki?
 
Inashangaza watu unakomaa kukanusha habari za wamachinga kulazimishwa kufunga maduka ili washiriki maombolezo ya kitaifa huku unaacha kukanusha kama kweli au si kweli watu 45 wamefariki na wengine mamia kujerujiwa.

Huu sio wakati wa kuacha kuwapa watanzania ukweli juu ya nini kinaendelea hapa nchini please nenda na matukio na wakati.View attachment 1731840
Naandika haya nikiwa na simanzi. Wamefariki watu zaidi ya 50. Yes hamsini. Leo nilikuwa Muhimbili kuchukuwa maiti za ndugu zetu. Nasema maiti za ndugu zetu kwani tulikuwa tunachukuwa maiti 4 za familia moja. Wanakwenda kuzikwa Tanga kesho. Mochwari imefurika. Watu ni zaidi ya hamsini. Bado Temeke hospital. Tumekuta familia nyingine imepoteza watu watano. Mama, watoto wanne na house girl. Serikali haijali. Haitoi msaada wowote.
 
Back
Top Bottom