Rc Kunenge tuambie ukweli juu ya vifo na idadi kamili iliyotokana na mkanyagano uwanja wa uhuru

Hii haifai kabisa, alafu mkuu wa mkoa anakaa kimya kama vile hakuna tatizo. Kwa serikali makini hata gharama za mazishi zilitakiwa kugharamiwa na serikali.
 
Wamekataa kutoa data za maambukizi na vifo kwenye Covid karibu mwaka sasa.

Wanaendeleza uzi ule ule.
 
Mshana Jr atuambie kama ni kafara.
 
Hivi kweli Jambo la kuchukua tahadhhari dhidi ya usalama wako, sio kichaa unahitaji kuambiwa na mtu?
Tuwe serious hata na post zetu na tusiwe wepesi was kulaumu kuliko uhalisia
 
Hivi kweli Jambo la kuchukua tahadhhari dhidi ya usalama wako, sio kichaa unahitaji kuambiwa na mtu?
Tuwe serious hata na post zetu na tusiwe wepesi was kulaumu kuliko uhalisia
Stampede/ mkanyagano ili kuzuiwa ilipaswa kamati ya mazishi iandae mazingira salama kwa waombolezaji ikiwa na kuhakikisha hakutakuwa na mtu kuvuruga foleni. Pia ilipaswa ifahamu capacity ya uwanja kisha kudhibiti watu walio nje namna ya kuingia.
 
Bora leo Dodoma wamefuata ushauri, Kwa umati Ile labda wangeaga wiki nzima. Kote kulikobaki Marehemu apitishwe Barabara kuu watu wapunge mikono. Inatosha Sana Tu.
Mungu awarehemu tu wafiwa kwakweli, binafsi sioni haja ya kutangaza chochote kwasasa maana wananchi wenyewe ndio walikua wakaidi wa maagizo ya jeshi la polisi.
 
Wangebaki manyumbani Serikali ingekuja kuwatoa kwa mtutu? Binadamu lazima uwe na uwezo wa kufanya risk assessment angalau level 1 kabla ya kuchukua maaamuzi yoyote kuhusiana na maisha yako na watu wako. If you can't do that don't expect the Government to do for you. Walienda uwanjani wenyewe wacha wabebe wajibu huo. Samahani kuongea hivi lakini ndiyo ukweli wenyewe
 
Hata mimi siungi mkono waliokwenda huko hasa wale waliokwenda na watoto tena wadogo kabisa. Au kama mtu umeenda angalau ukiona kuna umati mkubwa inabidi urudi. Lakini kusema waache wabebe msalaba wao siyo vizuri Serikali ndiyo ilihimiza watu wajitokeze kwa wingi lakini haikuandaa utaratibu mzuri. Wao waliitikia wito kumbe waliowaita hawawajali ila wanataka kuwatumia tu. Na ukichambua haraka haraka unaweza kukuta waliofariki wengi ni watu wenye maisha duni na pengine elimu ndogo. Sehemu kama pale sijui kama utawakuta wakazi wa Oysterbay, Masaki etc. Ni somo tosha japo limesomeshwa kwa gharama ya vifo vya vya watu zaidi ya 50.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…