The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack amewataka Halmashauri ya Mtama kuhakikisha wanawasimamaia fedha za miradi ya ujenzi wa shule na miundombinu ya elimu.
Telack ametoa wito huo mapema alipotembelea kukagua ujenzi wa shule na miundombinu hiyo ya elimu yenye thamani ya Bilioni 7.8
Soma pia: Pre GE2025 Miradi kuelekea Uchaguzi Mkuu: Mhandisi Kundo akagua mradi wa maji unaonufaisha zaidi ya wakazi 200,000 Chalinze
Kati ya fedha hizo, shilingi Bilioni 4.1 zinatoka serikali kuu, bilioni 3 kutoka kwenye Mradi wa Kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP), na milioni 719 kutoka kwenye Mradi wa Kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji kwa Shule za Awali na Msingi Tanzania Bara (BOOST).
Miradi inayotarajiwa kutekelezwa ni pamoja na ujenzi wa shule ya wavulana kanda ya Kiwalala, ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu sita ya choo katika Shule ya Msingi Mahumbika, ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na matundu sita ya choo katika Shule ya Msingi Chiuta, na ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu sita ya choo katika Shule ya Msingi Mandwanga.