RC Makalla: Machinga wote Dar walio katika hifadhi ya barabara, Wataondolewa na vibanda vyao kuanzia Septemba 13, 2021

Niombe chama tawala kwa dharura waingilie kati swala la hawa wamachinga wanaopambani haki zao wakiwa uchi hapo Kariakoo.

Nadhani RC Makalla hajaeleweka vizuri hivyo chama kiingilie kati kuokoa jahazi.

cc: Mzee Mgaya
Akili fupi Makala toa takataka hizo
 
Sioni mafanikio kwenye haya maamuzi. Wizi, na vurugu vitaongezeka kwa haraka sana.

Wangeanza kutenga machinga streets ndani ya Kariakoo huko huko na Posta ili maeneo mengine yaachwe bila vurugu.
 
Tatizo huyu mkulu matamko mengi, utekelezaji zero. Tungoje hili labda litatekelezwa.
 
Leo hii umegeuka reporter wa ccm
Hakika kazi ya ccm imeonekana
 
Mwendazake alituachia msala mkubwa sana, dar, mwanza, Arusha, Mbeya ni kero sana hata hamu ya kwenda kufanya manunuzi haipo tena

Wewe unafikiria kwa nini ilifikia hapa na mpaka akawapa vitambulisho vya 20,000/-? Sasa'asitokee mtu akataka kujisahaulisha haya. RC Makalla anatakiwa ajue anapowaondoa anawapeleka wapi kwenye wateja? Waelimishwe waelewe faida ya wao kuhamishwa wanapo hamishiwa na hiyo faida iwepo kweli isiwe ni nadharia tu. Wawahamishe kwa awamu na wale wanaobaki wakisubiria kuhamishiwa mahali mwafaka wajiridhishe wenzao ambao wameshahama maisha yanaendelea. Hii ndio moja ya kazi ya kiongozi kuonesha njia ya suluhisho la matatizo ya unaowaongoza. Vinginevo ikitumika nguvu kwa vile iko tutarajie majanga.
 
Hilo najua. Mimi kero yangu kubwa Dar ni joto. Hilo nadhani ni pote. Then kama hauna usafiri binafsi kwenye usafiri wa public ni hovyo sana sio daladala wala mwendokasi.
Kama ni joto kuna baadhi ya maeneo ya dar yana hali ya hewa karibu sawa na Iringa. Nimewahi kwenda King'ongo watu wanavaa masweta kabisa.
 
Walipe kodi inayostahili kutumia kuboresha vitambulisho vyao wataondoka wenyewe
 
Safi sana, kimsingi Kariakoo kwa sasa inapaswa ihamie Maeneo ya MBEZI MWISHO, STENDI YA MAGUFULI.

JIJI la DSM ljnapaswa lipanuke, tubadilike, wataalamu wa mipango miji wapo lkn hawataki kutumia taaluma zao vyema.
Mkuu kimsingi machinga biashara zao ni za kutembeza, hao wenye vibanda vya damu ya mzee ni wafanya biashara kama wafanyabiashara ambao wamepanga kwenye myumba za watu na wengine wana mali za mtaji mkubwa tu ila wanakwepa kulipa kodi, pango za kupangisha nyumba nk. Mfano utawakuta wengine wanakonteina la vinywaji (bia, soda nk) lenye mtaji mkubwa na anauza kuliko mwenye leseni ya bar ambaye analipa pango la nyumba ya biashara. Machinga feki mwingine utamkuta ana kakibanda chake cha bati ngumu amejaza spea za magari zenye mtaji mkumbwa kuwashinda hata wale wanaouza spea ambao wanalipa kodi zote. Ni wakati sasa wa TRA kuwatambua watu hawa. Kwa lugha ya kiuchumu ni kwamba utitiri huu wa wajasiliamali waliojibatiza jina la wamachanga ili wakwepe kulipa kodi za Serikali ni wengi sana ndio wanao sababisha Serikali kukosa fedha za kodi maana hawa ni wengi na halipi kodi. Serikali iwajengee sehemu za biashara ili walipe kodi, wapo wengi hivyo makusanyo ya kodi yatakuwa makubwa sana ili iwe mbadala wa hizi TOZO
 
Pale Mbezi maeneo ya CRDB Jamaa wakaona haitoshi wameamua kuweka mabanda yao barabarani kabisa. Magari ndiyo yanafanya kukwepa biashara zao.
Mkuu Mbezi inatisha kwa hawa watu, wamevamia kwelikweli utazani Mbezi kuna machimbo ya madini. Imepabwa na vibanda vyenye maturubai chakavu/mabovu. Ukiwaangalia kwa haraka haraka utadhani wamepewa vibali vya kuendesha biashara sehemu hizo.
 
Makalla akifanikiwa baada ya hiyo wiki alkiyotoa basi nitamnunulia beer.....
na nyamachoma count on me, hili ni jambo gumu sana kiutekelezaji maana limelelewa awamu kwa awamu na limekua sugu, linahitaji sera ya kitaifa na kuungwa mkono na serikali yote na wapenda ustaarabu.

Kila la heri Makalla, mwenyekiti chake akitengua maagizo haya kwa simu tu umeumia, si unajua ni msikivu na huwa anasikiliza zile huziita "kelele"?!
 
Usidanganyike wewe.

Machinga ndio wapiga kura wa CCM na wako kimkakati.

Subiri tamko kutoka juu kwamba Machinga wasibughuziwe!
Machinga hawajawahi kuwa wapiga kura wa mtu yeyote yule, aliyesema machinga ni wapiga kura wake alitafuta kushangiliwa tu.

Kura za CCM zipo vijijini si kwa wamachinga. Kuendelea kuwalea kwa kudhani ni wapiga kura ni kujidanganya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…