RC Makalla: Machinga wote Dar walio katika hifadhi ya barabara, Wataondolewa na vibanda vyao kuanzia Septemba 13, 2021

Bigupa kwa kuwapa muda ili waangalie ustaarabu wao mapema.

Ushauri;
Baadhi ya barabara au maeneo ya wazi kama jangwani yaandaliwe kwaajili ya machinga.
Au
Machinga wahamishiwe kwenye lile jengo lao kwa kodi ya pango nafuu.
Au
Yatengwe maeneo maalumu kwaajili ya machinga kufanya biashara kwa mtindo wa gulio. Mfano; j3, j. 5, ijumaa & j.2
machinga waachiwe wauze bidhaa zao kwenye baadhi ya maeneo yatakayotengwa. Kariakoo wanaweza wakaachiwa siku ya j.pili 0600-1800hrs. J.3 Ubungo-Manzese, J.5 Mwenge na Makumbusho,
Ijumaa wawe Taifa.
 
Viongozi wa mamlaka za Jiji ni wahalifu kwa kutenda au kutotenda kwa makusudi kuhusu uwepo wa wamachinga sehemu zisizoruhusiwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za mipango miji.
Jambo la kwanza linalotakiwa ni kuwawajibisha halafu utekelezaji wa sheria uendelee.
Ni upumbavu mkubwa kuvunja sheria na kanuni kwa sababu za kisiasa.
 
Ni jambo jema sana ,wamachinga na bodaboda wanazuia njia sana yaani ni kero tupu.

Makalla ameamua jambo jema ,wamachinga na bodaboda wakae kwa mpangilio na sehemu maalum.
 
Kuna jamaa hapo kushoto kaviiimba tumbo ka mpira wa criket
 
Ukimaliza hao, anza na magereji na park8ng za malori ya mizigo sehemu maeneo ya makazi
 
Narudia tena wewe unalipwa hapo hujui maana ya machinga.... machinga hawawezi kaa mbali ya wateja... wanatakiwa kuwa mjini... hayo maeneo unayo yataja ni yapi? machinga complex? Tusubiri afanikiwe nikuletee zawadi...... uwezi kuwatoa machinga mjini

Hakuna nchi hapa East Africa ni maskini kuliko sisi kwa hali zote yaani kifedha na kirasilimali ambazo hazina wamachinga kabisa kwny miji yao?
 
Hakuna nchi hapa East Africa ni maskini kuliko sisi kwa hali zote yaani kifedha na kirasilimali ambazo hazina wamachinga kabisa kwny miji yao?
Mkuu suala hapa sio kuwafukuza wamachinga bali nikuwapanga vizuri katika maeneo yao ya kazi. Aidha wengi wa wamachinga unaowaona leo wanafanya umachinga kwa niaba ya wafanyabiashara wakubwa ambao wanakwepa kulipa kodi na malipo ya leseni mbalimbali za kibiashara za kuamua kuwapatia hao wachinga.
 
HII SASA NDO KAZI NZURI.
Hao machinga wakiondolewa serikali ina uwezo wa kupata pesa nyingi zaidi kupitia parking za magari yatakayopaki humo barabarani, lakini pia wafabyabiashara wenye maduka wana uwezo wa kuuza zaidi na kuweza kulipa kodi zaidi. Na pia mandhari ya kariakoo itakaa sawa. Nshaachaga kwenda kariakoo lakini sasa nitaanza tena kwenda kama hao wakwangua magari na wavuta watu mashati kuwalazimisha kununua wataondoka.
Soko la Kisutu ndio mfano halisi sasa wa soko lenye mandharin nzuri. Ukiingia ndani ya soko la kisutu unatamani ukae siku nzima. Na kariakoo ifike mahali paeleweke na pawe na mpangilio mzuri kama ilivo kisutu sasa
 
Ndani ya Kariakoo unawapanga wapi?
 
Ndani ya kariakoo unawapanga wapi?
Mkuu Tough lady hawa watu tunao wazungumza wamachinga sio wa Kariakoko tu ni Dar yote kama sio Tanzania mzima. Wanatakiwa wapangwe kwa mujibu na taratibu za kisheria, na ionekane kweli ni mmachinga kweli na si mmachinga kwa mbinu za kukwepa KODI
 
Ila Dar sijui kwanin kunakuwaga vile, sijui ndio tuaeme maisha ni magumu kwa kila mtanzania, yaan wafanya biashara imekuwa kero wameijaza miji kwa vibiashara vya uchuuzi na vitu vidogovidogo ata kama ndio rizki lakin patengwe maeneo ya wamachinga ila sio kwa fujo iyo ya dar
 
Nampongeza kwa hili
Hata Mh Paul Makonda aliwapiga marufuku hao wafanyabiashara na tamko la Mwanza likapindua meza na yeye kushindwa katika zoezi hilo! Sasa huyu nae amesema hivyo kama Mh Hagaya hana taarifa, basi hili nalo ni katika kutengeneza tatizo na wao wenyewe kulirekebisha na sie kushangilia tu!!
 
Leo ni Terehe 5 mwezi wa 10 wamachinga bado wapo barabarani.
Haya matamko mengine ni ya kipumbavu Kama hayatekelezeki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…