#COVID19 RC Makalla, wananchi jitokezeni kupata chanjo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametoa wito kwa Wananchi kuhakikisha wanapokea Chanjo ya Corona kwa mustakabali wa Afya zao.

RC Makalla ametoa kauli hiyo akiwa ni miongoni mwa Viongozi waliopokea Chanjo hiyo wakati wa uzinduzi uliofanyika siku ya Jana ambapo amesema tangu amepokea Chanjo hiyo hajapata madhara yoyote ya kiafya.

Aidha RC Makalla amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuonyesha mfano kwa kuchanja na kutimiza wajibu wake wa kuwaletea wananchi Chanjo ili Waweze kuchanja kwa hiyari.

Pamoja na hayo RC Makalla ameendelea kuwasisitiza Wananchi kuchukuwa tahadhari dhidi ya Corona huku akisisitiza uvaaji wa Barakoa wawapo kwenye Vyombo vya usafiri na suala la Level seat.

Hayo yote yamejiri wakati wa ufunguzi wa Kikao Cha tathimini ya Lishe Mkoa wa Dar es salaam kilichohudhuriwa pia na Waziri wa Afya Mhe. Doroth Gwajima.

Akizungumza Katika kikao hicho RC Makalla amezielekeza Halmashauri zote za Mkoa huo kuhakikisha zinatenga fedha za kuwawezesha Maafisa Lishe kutekeleza majukumu yao.

Hata hivyo RC Makalla amewataka Maafisa Lishe kuhakikisha wanatoa Elimu ya kutosha kwa Wananchi kuhusu suala zima la Lishe ili kuepuka magonjwa mbalimbali ikiwemo Udumavu na utapiamlo.

Itakumbukwa kuwa Wakuu wa Mikoa yote nchini walisaini mikataba ya uboreshaji wa Lishe Katika maeneo yao kwa lengo la kuhakikisha jamii inakuwa na Afya Bora na Lishe Bora.
 
Chanjo ni hiari. Unataka chanjwa, hutaki acha wewe na familia yako. Bado haitoshi tu?

Kwamba unatafuta kuungwa mkono kutochanjwa? Kwani inakuuma nini wewe mtu akichanjwa au asipochanjwa?

Hiiiiii bagosha!
Unajua tuko tofauti katika mengi. Nikikutana na wewe unaelekea sehemu daraja livejunjika, ama kuna watekaji, nitakuambia usipite huko kuna madhara. Nandiyo sababu ninawapa watu anuani za kuapta kinga na tiba ya Corona kwa kuwa imethibitishwa. Sina uchoyo!.
 
Hizi ngonjera za nini sasa? Wao si waseme tu chanjo wapi na lini sisi tukafanye yetu?
 
Hapana kijana wangu. Ninahuruma na wanaoangamia. Kama ulivyomsaidia yule rafiki yako wakati mkisoma ili asifukuzwe ama kufeli, ilikuwa haikuhusu lakini ulimuwazia mema na ndiyo sababu ukamsaidia. Ndivyo na mimi nilivyo.
Chanjo ni hiari. Unataka chanjwa, hutaki acha wewe na familia yako. Bado haitoshi tu?

Kwamba unatafuta kuungwa mkono kutochanjwa? Kwani inakuuma nini wewe mtu akichanjwa au asipochanjwa?

Hiiiiii bagosha!
 
Vijiwe vya kahawa vimeanza kuchangamka....

Wadau wamepata uelewa mkubwa baada ya ufafanuzi wa mh.Rais na Waziri wa afya....

Wameanza kuhamasika....
Tumeanza kuhamasika.....


#TujitokezeniKuchanjwa
#ChanjoNiBoraKulikoTiba
#JMTMilele
#KaziIendelee
 
Binafsi nimeajindaa vyema kujitokeza kuchanjwa.

Nimemuelewa vyema mh.Rais na Waziri wetu wa afya Dr.Gwajima.

Nami ndani ya mwili wangu nina chanjo kadhaa ,kwanini niikatae chanjo hii ya UVIKO?

#NitajitokezaKuchanjwa
 
Hapana kijana wangu. Ninahuruma na wanaoangamia. Kama ulivyomsaidia yule rafiki yako wakati mkisoma ili asifukuzwe ama kufeli, ilikuwa haikuhusu lakini ulimuwazia mema na ndiyo sababu ukamsaidia. Ndivyo na mimi nilivyo.

Tafadhali usituhurumie. Acha tufe. SSH kasema yeye ni mama, bibi, mke, rais na amiri jeshi mkuu. Wewe ndiyo umhurumie?

Acheni kujikita machozi ya mamba. Tukisha kufa nchi itakuwa yenu CCM peke yenu shida gani jombi πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚?
 
Chanjo zenyewe Dose Mil. 1 na waTz tupo Mil. Appx. 60 sasa tujitokeze vipi
 
Watoe maelezo yaliyokamilika basi......


Lini wanaanza kuchanja na hospitali zipi


Kila mtu anaimba ngoma ya kuchanja maelezo ya kina hakuna!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…