RC Makonda avamia Clouds na kuwatisha SHILAWADU

Badala ya Gwajima kuchafuliwa nadhani yeye ndio anazama zaidi, itabidi shilawadu wamuulize yule mwanamke amelipwa sh. ngapi?

Hivi hizo studio hazina CCTV camera ambazo zimerekodi huo umafia Wa Mtoto Wa mfalme?
Kwa hiyo unatuambia kuwa Gwajima naye amelipwa shilingi ngapi kumchafua Makonda?

Hakuna aliye msafi chini ya jua, hivyo kuwa makini sana unapo msakama mwenzio ukianzia na wewe unayesoma hapa, vile ya kwako hayajawekwa hadharani haikufanyi innocent.

Askofu naamini huyu mtoto wa kwake, maana anapenda sana totoz, kumbuka mke wa Mbasha....
 
hivi seriously kuna mijitu ina quote story nzima alafu comment yenyewe maneno mawili tu! Why cant you just click "reply" tu
 
Makonda hua anafika office za clouds mara kwa mara. Siku zingine anashinda hapo mpaka jioni. Siku ya Alhamis Makonda alifika office za Clouds Cha ajabu siku hiyo alikaa mpaka usiku akawa anamtafuta soudy Brown na Qwisser wa SHILAWADU muda huo walikuwa bado hawajafika kazini basi akawa anazungukazunguka tu ofisi hii anatokea ile kama mfanyakazi wa Clouds.

Kwenye Mida ya Saa kumi hivi akakutana na kina Soudy pamoja na prodyuza wa kipindi wakawa wanaongea kwa uficho hivi na usiri tukajua tu ni mambo ya kawaida ya kuhitaji uprivate lakini siku ile ulikuwa unatia mashaka sana.

Kumbe Makonda alikuja na Story ya mwanamke mmoja ambaye yeye Makonda alisema huyo mwanamke amezaa na mchungaji Gwajima na ametelekeza akawa anataka arekodiwe na ubuyu uruke kwenye kipindi cha SHILAWADU.

Basi wakakubalia kwa kuwa ni habari itabidi huyo mwanamke arekodiwe na kipindi kiruke siku ya jana lakini kawaida ya Kipindi cha SHILAWADU ubuyu ukipatikana lazima kila mtu apewe Natural Justice ya kusikilizwa pande zote mbili sababu huwa ndiyo kawaida ya kipindi.

Makonda siku hiyo hiyo ya Alhamisi akamwambia Soudy ajiandae then huyo mwanamke mnayemuona kwenye video na mtoto aliletwa na wasaidizi wa Makonda ahojiwe na Soudy Brown tayari kwa kurushwa kwa kipindi.

Siku ya Ijumaa ambayo ilikuwa ni jana SHILAWADU wakamtafuta Gwajima kwa upande wake kama anaifahamu hiyo ishu na je mwanamke huyo aliyetajwa ni kweli kwasababu tunaelewa ugomvi uliopo kati ya Makonda na Gwajima isijekuwa SHILAWADU wanatumika kuwafitinisha watu vibaya!

kwa bahati mbaya Gwajima hakupatikana jana ijumaa kwa ajili ya kurekodiwa na kufanyiwa mahojiano.

SHILAWADU wakatumia busara mpaka apatikane Gwajima scene ya Dada mwenye mtoto ziende kwa pamoja na ya mchungaji Gwajima kama kawaida ya POVU inavyokuwaga.

Jana usiku sasa kumbe Makonda alikuwa anafuatilia kipindi cha SHILAWADU aone kama kile kipande kitaruka hewani wapi ndiyo akaamua kuja Clouds na magari mawili yeye mwenyewe Makonda na Watu kama nane hivi wakiwa na Bunduki aina ya SMG geti la kawaida mlinzi alifungua geti kwasababu amezoeleka Mh anakujaga mjengoni wakafunguliwa kisha wakaingia ndani.

Walipofika reception wakazuiwa kuingia ndani sababu hatuna utaratibu wa kuruhusu wageni baada ya saa Nne usiku kuingia ndani ya Ofisi kama siyo mfanyakazi wa CLOUDS.

Alipoona wanazuiwa wakatoa bunduki zao mlinzi akashurutishwa afungue mlango kwa nguvu sababu walimtishia na Silaha mlimzi akafungua mlango wakaenda naye hadi studio kipindi kilikuwa kinaendelea hewani.

Makonda akawatoa nje Soudy na Mwenzake Qwisser akawauliza kwanini video aliyowaletea haijachezwa wakaelezea utaratibu jinsi utaratibu ulivyokuwa Qwisser wakati anajielezea akapigwa mtama akaanguka chini wakavamia mitambo ya transmission kwenye traycaster wakitaka kile kipande kirushwe hewani prodyuza wa kipindi akamuambia Makonda kwanini anavunja utaratibu na kutumia nguvu na ameshapewa utaratibu akapigwa na kitako cha Bunduki mgongoni akaanguka chini bahati mbaya kipindi kilikuwa kimefika mwisho.

Wakamshurutisha Prodyuza wa SHILAWADU anaitwa Chriss awape kile kipande wakaondoka naye wakati wanaondoka Ruge alikuja na Polisi akaingia lakini tayari walikuwa wameondoka ofisini wamechukua hicho kipande cha Video ya huyo mwanamke.

Hizo video zilichukuliwa kwa nguvu na Makonda na hao watu waliokuwa na Silaha inasemekana Makonda ana timu yake wanazisambaza kwa kasi na hatujui lengo lake ni nini.

Hata mkihitaji footage za Camera zipo jinsi tukio lilivyokuwa usiku wa jana.

 
Huyu Bashite mwaka huu kala maharage ya wapi?

Hamumuachi tu?


Njoo ufanyiwe maombi - By Bonny Mwaitege


Bashite karibu kanisani kwetu Ubungo kesho

Kama kweli huwa unafuata maombi kanisani na sio u.......!!!
 
Weka hiyo footage ili habari hii isisalie kuwa uzushi
 
"SMALL AXE" Bob Marley
"CRAZY WORLD" Lucky Dube
"THE WAY IT IS" -Lucky Dube ( a gift )
 
Nahitaji hizo camera footages nihakikishe
 
That's none of our business, sisi tunachohitaji vyeti vya kiongozi wetu, Gwajima atajuana na 'familia' yake
 
mbona kadi haina jina la klinik anapo pimiwa mtoto? au nayo magumashi?
 
Kwa watu wenye akili "nyingi sana" hupenda kuendesha siasa zao kwa kutumia akili sana, lakini kwa bahati mbaya kundi kubwa sana la watu walio kwenye siasa si watu wenye hizo akili "nyingi sana" na ndiyo maana hao watu wenye hizo akili huwa hawaoni kinachoonwa na jamii pana na Jamii husika huwa haioni kinachoonwa na hao wasomi.

Tanzania hivi sasa imeonekana wasanii wa pande pili wakitumika kujenga taswira kuwa upande mmoja wa kundi la siasa unashinda kwa kuvuta watu wengi sana. Kuna watu wanapoamka tu ni lazima waangalie kwenye kurasa ya Instagram ya Mange kimambi kaandika nini. Lakini kuna watu pia wanawashangaa hao wenzao wanapata nini kwa Mange kimambi.

Lakini lipo pia kundi ambalo halilali mpaka liangalie Shilawadu na kwenye shilawadu huwezi kuona makala nyingi zenye kuashiria kushadadia ama watu wa vyama vya upinzania ama wasanii wanaojihusisha na upinzania. Kuna kundi linaloona SHILAWADU ni mkakati wa watawala dhidi ya wapinzani wao.

Kwa mtazamo wangu Mange kimambi na SHILAWADU ni aina ya nguvu inayotumika katika siasa za nchi yetu kuvuta mashabiki. Huwezi kuona kwa hivi sasa Mange Kimambi akisifiwa na watawala kwa "kufichua" Maovu ama kuona wapinzani wakikisifu kipindi cha SHILAWADU kwa kuiweka "sawa" jamii ya kitanzania. Kuna nguvu iko kwa Mange Kimambi na SHILAWADU kwenye mzingo wa siasa za Tanzania!
 
PINDI MTU ANAPOTAFUTA KUPIGWA TOFARI LA KICHWA....NGOJA NIKAE KIMYA NIONE KITAKACHOJILI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…