johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
RC Makonda amemkaribisha Katibu mkuu wa CCM Dr Nchimbi mkoani Arusha na kumhakikishia makamisaa wanachapa Kazi
Aidha Makonda amesema kwa sasa yeye na Waziri Silaa Wanafanya Kazi kubwa ya kutatua migogoro ya Ardhi na kwamba Waziri Silaa anafanya Kazi iliyotukuka
Source: Ayo TV
====
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amemuhakikishia Katibu Mkuu wa CCM, Emmanuel Nchimbi kwamba Serikali Mkoani humo inaendelea kutekeleza yaliyoelekezwa kwenye Ilani ya CCM ambapo amesema Viongozi wa Mkoa huo wanaendelea kufanya kazi yao vizuri na wale wasiochapa kazi anawapiga spana kwelikweli.
Akiongea leo June 02,2024 Mkoani Arusha Makonda amesema “Mh. Katibu Mkuu, mkutano huu ni wa kwako, sisi upande wa Serikali tunafanya kila iwezekanavyo kuhakikisha kwamba tunatekeleza mliyotuelekeza kwa mujibu wa Ilani 2020/2025 kama ulivyoona Makamisaa waliopo hapa wanaendelea kufanya kazi yao vizuri, wanachapa kazi na wale wasiochapa kazi ninawapiga spana kwelikweli kuhakikisha kile mnachotaka kifanyike kinafanyika kikamilifu”
“Ipo changamoto kwenye Mkoa wetu, changamoto namba moja ni migogoro ya ardhi lakini nikuhakikishie chini ya Waziri wetu Comrade Jerry Silaa na Mimi nikiwa RC wa Arusha tunahakikisha kila mwenye haki anapata haki yake”