The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima ameitaka Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Morogoro kuhakikisha inafanya ukarabati wa madaraja yote na miundombinu ya barabara mbovu zinaounganisha Mkoa huo ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza wakati mvua zitakapoanza kunyesha.
Malima amesema hayo Machi 4, 2025 katika kikao cha Bodi ya Barabara mkoani humo ambapo amesisitiza kuwa mkoa wa Morogoro ni miongoni mwa mikoa inayoathiriwa sana na mafuriko hivyo uboreshaji wa miundombinu na madaraja kutasaidia kuondoa changamoto hiyo.
Pia amesema serikali inakusudia kufungua barabara zote za mkoa wa Morogoro na mikoa ya jirani ili kukuza uchumi kati ya wananchi wa mkoa wa Morogoro na mikoa mingine ikiwa ni sehemu ya kufungua fursa za kibiashara.
Kwa upande wao baadhi ya wabunge waliohudhuria kikao hicho, Godwin Kunambi na Christina Ishengoma wamesema kuwa ujenzi wa barabara zinazounganisha mkoa wa Morogoro na mikoa jirani zitasaidia kuinua uchumi kwa wakazi wa mkoa huo, ikiwemo kurahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa ikiwemo mazao ya kilimo.
Naye Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro Mhandisi John Mkumbo amesema kuwa tayari Wakala ya Barabara ya Mkoa huo imeanza kufanya mchakatao utakaowezesha upatikanaji wa wakandarasi kwa lengo la kuanza kazi ya kuboresha na kujenga miundombinu ya barabara katika mkoa huo.