LGE2024 RC Malima: Mume haruhusiwi kumkataza mke kujiandikisha, akibainika atakamatwa

LGE2024 RC Malima: Mume haruhusiwi kumkataza mke kujiandikisha, akibainika atakamatwa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

the guardian 17

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
395
Reaction score
570
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima ametoa onyo kwa mtu yeyote atakayeleta vurugu ili kukwamisha zoezi la uandikishaji wa wapiga kura serikali za mitaa unaoendelea kufanyika Mkoani humo na nchi nzima kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari RC Malima amesema kuwa vyombo vya ulinzi vimeimarisha ulinzi katika maeneo yote zoezi linakofanyika ambapo amebainisha kuwa mtu haruhusiwi kushawishi watu wengine kususia zoezi hilo hata kama ni Mume haruhusiwi kushawishi mke asijiandikishe na akifanya hivyo atakamatwa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Yusuph Makunja amewaasa vijana Wilayani humo kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili waweze kuwachangua viongozi wanaowataka watakao kuwa msaada kuleta maendeleo na kuwawakilisha katika ngazi mbalimbali.
 
huyu jamaa nakumbuka alipandishwa mahakamani huyu kipindi cha Magu alileta kujuana kwenye kazi
 
Back
Top Bottom