RC Manyara, Queen Sendiga Akabidhiwa Nyumba 74 za Waathirika wa Maporomoko ya Matope

RC Manyara, Queen Sendiga Akabidhiwa Nyumba 74 za Waathirika wa Maporomoko ya Matope

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

GUR3NAUXoAA5pkp.jpg

Agosti 5, 2024 kumefanyika makabidhiano ya mradi wa ujenzi wa nyumba 74 za waathirika wa maporomoko ya matope zilizopo katika eneo la Warret Wilayani Hanang kati ya Suma JKT na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara

Ujenzi umekamilika kwa asilimia mia moja (100%) ambao ulianza machi 18 2024 chini ya SUMA JKT. Nyumba zilizobaki 35 ziko kwenye hatua za umaliziaji ambazo zinajengwa na Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Sendiga amewapongeza Suma JKT, Halmashauri ya Wilaya ya Hanang na Mkuu wa Wilaya ya Hanang kwa kazi kubwa, ushirikiano na usimamizi katika kuhakikisha ujenzi wa nyumba hizi unakamilika katika ubora uliotakiwa.

GUOvionW4AAwIc3.jpg


Kwa niaba ya wananchi wa Manyara, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Sendiga ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha za ujenzi wa nyumba hizo.

GUOvgo9XgAALuYi.jpg
 

Attachments

  • GUOviHVWkAABkjO.jpg
    GUOviHVWkAABkjO.jpg
    102.8 KB · Views: 14
  • GUOvgm1WcAAYpDn.jpg
    GUOvgm1WcAAYpDn.jpg
    196.7 KB · Views: 14
Back
Top Bottom