Moshe Dayan
JF-Expert Member
- Feb 10, 2008
- 815
- 702
hivi mnaonaje RC's wakawa wanachaguliwa na wananchi wa mkoa husika na wawe wazawa au wana asili ya mkoa husika? nadhani watajitahidi kuhakikisha maendeleo mikoani mwao.kwa maana, wengi wetu hapa hata ukiuliza kazi za mkuu wa mkoa hatuzijui tunazijua za wabunge na watawala wengine wa mikoa.hii inatokana na michango yao midogo kwenye mikoa husika.na uchaguzi uwe labda after 5 years.
wengi wao huwa wanaishi Dar es salaam na kuacha mikoa yao.naomba mnisaidie, hivi dito alikua anashughuli gani dar alipopata ajali? mi nadhani wengi huchaguliwa kiswahiba, mnalionaje hili?
Unajua baada ya kuvunjwa kwa Azimio La Arusha, kama RC wa mkoa hawezi kuwa hela zake binafsi zinazozidi shillingi millioni 20, basi kama taifa tutakuwa na matatizo makubwa sana, maana huyo kiongozi itakuwa na maana kwamba hana biashara yoyote, hana shares za kibiashara mahali popote, hana hata kamradi kadogo dogo kakumuingizia extra money, meaning kwamba huyu mkuu hana any idea na uchumi hasa wa binafsi, sasa atauwezaje wa mkoa au taifa?
No wonder viongozi wetu siku zote ni magoi goi tu wakufuata bendera na kuogopa kuwa na misimamo imara kwa wananchi against wakubwa kwa kuogopa kufukuzwa kazi!
It is just sad and pathetic!
Bottom line bongo tunahitaji campaign finance // political contribution laws
Pengine hizo milioni 20 angepewa Mbowe ili zimsaidie kulipia deni lake....
ES kama ni hela zake na anachangia kivyake basi waseme hivyo na wasitumie cheo cha RC.
Halafu hapo ndipo watu watajua RC ana biashara gani na kama anaweza kuchangia hivyo au la.
Bottom line bongo tunahitaji campaign finance // political contribution laws .
Just out of curious,
Kwani sh. 20m ni hela nyingi sana kwa Mkuu wa Mkoa nazo? Nadhani hii ni hela anaweza kabisa kuitoa mfukoni mwake kama anataka kupalilia?
Naamini kuna afanyakazi wengie tu wa serikali wanaweza kuandika check ya sh. 20m bila shaka.
Hii siyo haki kwani naamini fedha hizo hajazitoa mfukoni mwake bali bajeti aliyotengewa na Tamisemi/wizara ya fedha kwa ajili ya kutekeleza mipango ya maendeleo ya wananchi.
Mkuu Pundit hao unaowasema ni kina nani? RC hawezi kutoa hela za mkoa si kuna wakaguzi wa serikali hupitia huko? Ina maana hela alizozitoa ni zake biinafsi, mbona hatujawahi kusikia kuwa ofisi imetoa tuu, unajua wakuu sometimes mnalaumu tu hata visivyolaumika,
RC hawezi kutoa shillingi millioni 20 za serikali bila mpangilio maaalum, zingekuwa za serikali ingesemwa, hizo mkuu ni zake binafsi je kuna tatizo?
Mkuu wa mkoa hebu tueleze hizo milioni 20 umezitoa wapi?Kwa mafungu ya RC's anayopewa kutoka serikalini na kutoa milioni 20 sio mchezo,hawa watu kifedha hawamsogelei mkurugenzi wa manispaa sasa huyu RC amezitoa wapi,mimi nadhani achunguzwe sio kawaida kwa RC kutoa hicho kiwango.Huyu RC anaweza kua miongoni mwa mafisadi.
Unajua alichokifanya huyo RC ni unafiki kwa Rais ili amuone anafaa na nafikiri hana sifa za kupewa U-RC aliupa kimiujiza hivyo anachofanya ni kujikombeleza kwa JK kwa kukiunga chama.Hili kacheza faulo mtu wangu.
Lakini RC yuko upande wa serikali kuu,hivi hapa hajachemsha?
You are absolutely right!
Lakini ziwe za mwanachama wa CCM na sio mwanachama halafu ni kiongozi kama RC.
Hivi huoni hapa pana walakini?
Wan JF nadhani sasa tuwe makini. Tuwe fair. Yaani tumeishafikia hatua ya kuwa every CCM leader is "Guilty until proven innocent"?
Nadhani si kosa kwa kiongozi kutoa mchango unless tuna uhakika au angalau wasi wasi kuwa si za halali. Lakini kuwa kiongozi wa CCM na kutoa mchango should not always be such a tragic combination.
Unaweza pia kuweka the other side ya hii story. Je hizo pesa amezitoa ni zake binafsi au ni za serikali. Kama ni za kwake binafsi, je ana biashara za kumwezesha kutoa hizo pesa? Haya ni maswali ambayo yanaulizwa na serikali nyingi duniani.
Hapa marekani unaweza kufanyiwa uchunguzi na FBI kama unaonekana kuwa unanunua vitu vinavyozidi vyanzo vyako vya mapato na kama haionyeshi kuwa umekopa hivyo vitu!