RC Morogoro azindua kampeni ya 'Jisomeshe na mkarafuu'

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mkoa wa Morogoro umezindua kampeni ya Jisomeshe na Mkarafuu, kampeni ambayo inawahusu wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Kampeni hiyo imezinduliwa katika kata ya Mkuyuni, Morogoro Vijijini, ambapo Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Dokta Mussa Ally Mussa, amesema wanafunzi 800 wamepatiwa miche kumi kila mmoja ya mkarafuu yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 5.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, ametoa onyo kwa wafanyabiashara ambao wananunua mazao ya viungo mkoani humo bila kufuata taratibu, na ameahidi kuwashughulikia.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde, amesema serikali itaweka utaratibu wa bei elekezi ambao utawawezesha wakulima kunufaika na mazao ya viungo tofauti na ilivyo sasa.

Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…