RC Morogoro, waondolee adha wanayopata wananchi wa tarafa ya Magole na kata ya Mbigiri

RC Morogoro, waondolee adha wanayopata wananchi wa tarafa ya Magole na kata ya Mbigiri

nguruka wa kig0ma

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2020
Posts
2,946
Reaction score
2,932
Kuna viongozi hawa wawili toka kwenye eneo hilo wamekuwa kero kubwa sana kwa wananchi wa eneo husika.

Maeneo haya mawili yapo kwenye tarafa moja na wilaya moja.

Ndg. Nchimbi ndiye mkuu wa Tarafa hiyo, lakini utawala wake ni wa fimbo ya chuma akishirikiana na polish dumila na wana CCM wa eneo hill.

Watangulizi wako, Kebwe na Saanane hata mkuu wa wilaya aliyeondoka walishindwa kung'oa kwa kumuhamisha au kumfukuza kazi, kwakuwa alikuwa anapora mashamba ya wakulima huko Mbigiri na Msowero kwa kushirikiana na mtendaji kata ya mbigiri na kuwagawia viongozi hao.

Kama haitoshi aliwakusanyia ng'ombe na fedha toka kwa wafugaji wa Kimasai I'll wafugaji wachunge mifugo yao kwenye eneo hilo ambalo idadi kubwa linatumiwa na wakulima.

Hivyo basi, hebu watafutie amani ya mioyo wananchi wako wa eneo hilo kwa kuwaondoa hawa viongozi wawili na kuwaletea viongozi wengine.

Nchi no mwiba kwenye eneo hilo.
 
Mkuu nimeona Msowero /Msovero.

Vipi ndio kipande ambacho chief mangungo alikiuza kwa Wajerumani au?
 
Ndg. Nchimbi ndiye mkuu wa Tarafa hiyo, lakini utawala wake ni wa fimbo ya chuma akishirikiana na polish dumila
Huyu Nchimbi hafai hata kuitwa ndugu, ni mnyama, mshenzi kabisa, mla rushwa mkubwa, anawahujumu sana wananchi kisa rushwa anazopewa na wafugaji akishirikiana na polisi, kiukweli kunatakiwa kufumuliwa kabisa mtandao uliopo kuanzia polisi, tarafa na baadhi ya watendaji wasio waadilifu, wananchi wanataabika kisa hawana mtetezi, ipo haja kuitishwe kura ya maoni kwa wananchi dhidi ya huo mtandao kandamizi wa polisi na nchimbi wao
 
Back
Top Bottom