RC Mtaka aagiza Halmashauri za Njombe kulipa Wenyeviti

RC Mtaka aagiza Halmashauri za Njombe kulipa Wenyeviti

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
9,524
Reaction score
13,682
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka ameagiza Halmashauri zote mkoani Njombe kuanza kuwalipa posho Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji kupitia mapato ya ndani.

Mtaka amesema mkoa wa Njombe hauwezi kushindwa kuwalipa Wenyeviti hao kwani halmashauri zake zinakusanya mapato kutoka katika vijiji na mitaa ambayo ndio wanayoiongoza Wenyeviti hao.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu Mkoa Anthony Mtaka Februari 14, 2025 alipofanya Mkutano na Wenyeviti wa Vijiji na Mitaa yote mkoa wa Njombe katika Ukumbi Uliopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
 
Wakati bajeti inapitishwa na Kamati ya Ushauri ya Mkoa, hilo fungu aliliona?
 
Wakati bajeti inapitishwa na Kamati ya Ushauri ya Mkoa, hilo fungu aliliona?
Sasa ndiyo wakati wa kupanga bajeti kwa hiyo anataka hilo fungu liwepo!
 
Sasa ndiyo wakati wa kupanga bajeti kwa hiyo anataka hilo fungu liwepo!
Bajeti unafata maelekezo ya Wizara ya Fedha, kama kuna commitment ya serikali katika hilo, litakubaliwa, otherwise ni kuwalaghai tu hao wahusika na pia ni siasa za kitapeli, anyway, sidhani kana bajeti bado iko ngazi ya wilaya au Mkoa, imeshapita
 
Halmashauri zinaruhusiwa kupanga mipango yao na kutekeleza kwa kutumia makusanyo yao ya ndani. Wizara ya fedha inatoa maelekezo ya matumizi ya fedha zinazotoka fungu kuu la Taifa.
 
Dah kweli keki ya taifa ni tamu naona wala inchi wameanza kuandaa mazingira ya kuwalaghai mazumbu kuku ili waendelee kula mema ya inchi peke yao na koo zao...
 
Mikoa kama njombe hasa kwa rejea ya pesa kupotea Bora kipi uwape posho wenyeviti au Kila mwaka kwenye ukaguzi wakute Milioni 500 zimepotea, seriously speaking Mtaka ameongea point muhimu sana
 
Hakuna watu hawathaminiwi kama kama wenyeviti lakini likitokea tatizo wao ndio wakwaza kuulizwa. Hivi serikali kwa kuwatumia wenyevit wangeweza kukusanya kodi kubwa kwenye ardhi. leo hii ni asilimia chache ya watanzania wanalipa kodi ya ardhi. Mwenyekiti wa mtaa/kijiji au kitongoji ni Kazi ya kujitolea haina posho wala mshahara na ni lazima uwe na kazi ya kukuingizia kipato. Hilo ni moja la sharti la uenyekit
 
CCM haijui kula na vipofu!
 
Back
Top Bottom